chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,834
- 26,217
MKURUGENZI wa Utetezi na Maboresho kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia, amesema adhabu ya kunyongwa inachangia kupoteza nguvu kazi nchini.
Sungusia alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipokuwa akitoa mada kwenye mkutano wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF).
Alisema pindi mtuhumiwa anapohukumiwa kunyongwa, nchi inakuwa inazidi kupoteza nguvu kazi, kwani na yeye tayari anakuwa ameshampoteza anayetuhumiwa kumuua.
"Adhabu ya kifo sio sahihi na kwanza haimjengi mtuhumiwa, kwani na yeye anapohukumiwa kunyongwa tunakuwa tunazidi kupoteza nguvu kazi ambayo ingeweza kuzalisha na kipato kikaendelea kusaidia wale waliobaki," alisema Sungusia.
Badala yake ameishauri serikali kuwatengea magereza maalumu watuhumiwa hao ambako watakuwa wakifanya shughuli za kuzalisha na kisha fedha zinazopatikana kuhifadhiwa kwenye mfuko ambao utawasaidia wajane na yatima wanaobaki.
" Si kwamba tunawatetea watuhumiwa wa mauaji, lakini adhabu ya kifo kwake haimsaidii, kwani unapomuua na yeye tayari unakuwa umepoteza nguvu kazi ambayo ingeweza kuzalisha kipato na kikasaidia wanaobaki kuliko adhabu ya kifo," alisema Sungusia.
Pamoja na mambo mengine, Sungusia aliitaka serikali kuruhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambayo ilizuiwa kwa muda usiojulikana kutokana na vurugu za gesi mwaka jana.
Source: Tanzania Daima