LHRC: Kuongezeka kwa Deni la Taifa kunaweza kuongeza ukali wa maisha, gharama za uendeshaji wa Serikali zipunguzwe

LHRC: Kuongezeka kwa Deni la Taifa kunaweza kuongeza ukali wa maisha, gharama za uendeshaji wa Serikali zipunguzwe

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
WhatsApp Image 2024-06-26 at 16.59.44_ddc906f8.jpg
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeeleza kwamba kuendelea kuongezeka kwa deni la Taifa kunaashiria kwamba ukali wa maisha unaweza kuongezeka ukisababishwa na kulipa deni hilo.

Ili kupunguza makali hayo wanashauri "Ni maoni yetu kuwa , ni muhimu kwa Serikali kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali ikiwemo posho, maisha ya kifahari na magari ya gharama kubwa ambayo yanaweza kuwa na mbadala wake"

Katika taarifa yao kwa umma kuhusu 'Mhutasari wa rahisi na maoni ya LHRC kuhusu Makadirio ya Mapendekezo ya Bajeti ya Serikali 2024/2025 kwa mtazamo wa Haki za Binadamu', inanukuliwa ikieleza kwamba kufikia Mwezi Machi, 2024 Deni la Taifa lilikuwa lmefikia Trilioni 91.7, ikilinganishwa na mwa 2022 ambapo deni lilikuwa Trilioni 69.44 kutoka Trilioni 60.72 mwaka 2021.

Aidha katika maoni yao wadau hao wameeleza kwamba katika jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Bajeti inakindhaba na jitihada za kimataifa kwa kutunza mazingira, kwa kuweka tozo kwenye gesi inatotumika kuendesha mitambo kama vile engine za magari na Bajaji, pamoja na kuweka kodi kwenye magari yanayotumia umeme.

Wamedai kuwa pendekezo hilo linarudisha nyuma lengo namba 13 la Maendeleo Endelevu ya Dunia, ambalo linaweka malengo madogo ya Nchi wanachama wa Ummoja wa Mataifa kuweka mipango ya kisera ili kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Wemedai kuwa inafahamika kuwa nishati ya umeme pamoja na gesi ni kati ya nishati zenye madhara ya chini kwenye kuzalisha hewa ukaa ikilinganishwa na mafuta ya petrol na dizel.

1 lh.jpg

2lh.jpg

3lh.jpg

4lh.jpg

6lh.jpg

7lh.jpg

8lh.jpg

9lh.jpg
 
Back
Top Bottom