Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa mamlaka zinazohusika na usimamizi wa haki kuhakikisha Dkt. Wilbroad Slaa anapatiwa haki yake ya dhamana, kufuatia kukamatwa kwake tarehe 9 Januari 2025 kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao.
Pia, Soma: Wakili Madeleka: Dkt. Wilbrod Slaa ataendelea kusota Magereza hadi Januari 30, 2025, kwa sababu; "Kuna ugeni wa Marais"
Dkt. Slaa alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya shauri la jinai Na. 993 la mwaka 2024, lakini alinyimwa dhamana.
TAARIFA KWA UMMA
WITO KWA MAMLAKA ZA USIMAMIZI WA HAKI KUMPA HAKI YA DHAMANA DKT. WILBROAD SLAA.
Dar es Salaam, 27 Januari 2025
Tarehe 9 Januari mwaka 2025 zililipotiwa taarifa kupitia vyombo vya habari za kukamatwa kwa mwanadiplomasia na mwanasiasa mkongwe Dkt. Wilbroad Slaa kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao Na.14 ya mwaka 2015. Siku hiyohiyo Dkt. Wilbroad Slaa alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupitia shauri la jinai Na. 993 la mwaka 2024 kujibu tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Katika hali ya kushangaza licha ya kosa hilo kutokuwa miongoni mwa makosa yasiyo na dhamana kama ilivyoanishwa katika kifungu cha 148(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura Na. 20 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2022, Dkt. Slaa alilipotiwa kukosa dhamana baada ya Jamhuri kuwasilisha shauri dogo la kuzuia dhamana.
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania dhamana ni haki ya kikatiba kama ilivyoanishwa katika ibara ya 13(6)(a) na 15 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sanjali na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa ambayo Tanzania ni nchi mwanachama.
Siku za hivi karibuni kumekuwepo na utamaduni wa vyombo vya upelelezi kuwasilisha viapo au mashauri madogo ya kuzuia dhamana kwa watu wanaotuhumiwa kuwa na makosa yenye mtazamo wa ukosoaji wa utendaji wa Serikali. Makosa mengi ya namna hii japokuwa kisheria yanastahili dhamana, kwa mfano kesi iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo ndugu Boniface Jacob; kada wa CHADEMA mkoa wa Tanga ndugu Kombo Mbwana na watanzania wengine wengi wamekuwa wakikosa haki ya dhamana.
Ikumbukwe kuwa, mwaka 2022 Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ilifanyiwa marekebisho kwa kuongeza kifungu cha 131A ambacho kilipiga marufuku Jamhuri kuwasilisha kesi mahakamani wakati upelelezi haujakamilika. Hivyo ni muhimu kwa Jamhuri kuzingatia sheria hii kwa kutowasilisha mashauri mahakamani kama upelelezi haujakamilika.
LHRC inatoa wito kama ifuatavyo:
1. Vyombo vya upelelezi nchini kuacha utamaduni wa kuzuia dhamana kwa makosa ambayo si miongoni mwa makosa yanayoangukia chini ya kifungu cha 148(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
2. Vyombo vya usimamizi wa haki kumpa haki ya dhamana Dkt. Wilbroad Slaa na watanzania wengine waliokutwa na madhila haya ya usimamizi wa haki jinai.
Imetolewa na:
Dkt. Anna Henga
Mkurugenzi Mtendaji- LHRC