LHRC, THRDC walaani mauaji ya mtoto mwenye ualibino wataka 'mnyororo' wa walioshiriki ubainike na kuwajibishwa

LHRC, THRDC walaani mauaji ya mtoto mwenye ualibino wataka 'mnyororo' wa walioshiriki ubainike na kuwajibishwa

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) nakwa pamoja wamelaani vikali tukio la lililotokea Wilayani Muleba mkoani Kagera la utekwaji na mauaji ya kikatili ya mtoto mwenye ualibino Asimwe Novath.
IMG-20240619-WA0004.jpg

Kufuatia tukio hilo wadau hao ambao ni Asasi za Kiraia leo Juni 19, 2024 wametoa tamko lenye wito kwa mamlaka, wadau pamoja na jamii kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya tukio hilo pamoja na kuwezesha mazingira rafiki kwa watu wenye ualibino nchini.

"Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hili na kuhakikisha kuwa wahusika wote, ikiwemo walioratibu utekelezaji, uuaji na watumiaji wa viungo vya watu hao na kuwafikisha kwenye vyombo vya Sheria haraka iwezekanavyo" wameeleza katika tamko hilo

Pia wito wao mwingine wameuelekeza kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) kuweka mikakati madhubuti ya kuwatambua na kusimamia ustawi wa watu wote wenye aalibino katika maeneo yote ya Nchi.

Vilevile wametoa wito kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutumia kipindi hiki cha Bajeti kujadili na kuweka fungu maalum ili kuimarisha mifumo ya ulinzi kwa watu wenye ualibino, katika ngazi zote kuanzia Kitangoji, Kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa hadi Kitaifa ikiwa lengo ni kuhakikisha maisha ya Watu wenye ualibino yanalindwa.

Aidha katika wito wao mwingine wameitaka jamii kutofumbia macho Watu wanaohusika na vitendo vya aina hiyo badala yake wawe mstari wa mbele kuripoti ili vyombo vya ulinzi na usalama viweze kuchukua hatua za upelelezi, lakini pia wamesisitiza jamii kuondokana na mila potofu juu ya matumizi ya viungo vya watu wenye ualibino kwa kuhusisha na utajiri au kujipatia mamlaka katika ngazi mbalimbali.

Hata hivyo katika tamko hilo wadau hao wameeleza kusikitishwa na namna mamlaka ilivyochulia tukio hilo baada ya kuripotiwa kutokea

"THRDC na LHRC hatujaridhishwa na mwitikio wa mamlaka husika ikiwemo kutoa taarifa kwa umma kujulisha jitahada zilichukuliwa punde baada ya taarifa ya kupotea kwa mtoto huyo, pia hakukuwa na taarifa yoyote kwa umma juu ya kuwatafuta watu waliofanya tukio hilo. Jambo hili linaongeza hofu kwa jamii ya watu wenye ualibino kuhusu usalama wao katika Nchi yenye amani na sifa ya kulinda haki za binadamu." wameeleza katika tamko la pamoja

Lakini pia katika tamko lao wameikumbusha Serikali kuwa, mapema mwaka huu, Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Watu wenye Ulemavu (CRPD) ilieleza maskitiko yake kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokuwa tayari kufuatilia maombi matatu yaliyowasilishwa kwenye Kamati hiyo kuhusu ukataji viungo vya watu wenye ualibino na kutowajibika kwa Tanzania dhidi ya matukio hayo.

Imeelezwa kwamba Kamati hiyo ilisema kwamba kushindwa kwa Tanzania kulaani na kuchunguza mashambulizi dhidi ya watu wenye ualibino kunaweza kuwa ni ukiukwaji wa wajibu wake wa kuwalinda watu wenye ulemavu.

Itakumbukwa jana Juni 18, 2024, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan alionesha kusikitishwa na kifo hicho kilichoripotiwa kutokea Jun 17, 2024 Kitongoji cha Mbale,Kijiji cha Bulamula, Kata ya Kamachumu mkoaniKagera, ambapo mwili wa mtoto huyo uliripotiwa kuokotwa ukiwa umeondolewa baadhi ya viungo.

PIA SOMA:
- Chama cha Watu wenye Ualibino Tanzania (TAS), THRDC walaani vikali tukio la kudaiwa kuvamiwa na kushambuliwa kwa mtoto mwenye ualibino Geita.

- Mtoto Asimwe Novath aliyekuwa na miaka miwili na miezi sita akutwa amefariki na mwili kufungwa kwenye mfuko

- Kifo cha mtoto albino kinataka amri ya Rais sio masikitiko ya Rais

- Tumeshindwa kumlinda Asimwe

- Kufuta mauaji ya albino, ni kutokomeza kabisa Waganga wapiga ramli
 
Back
Top Bottom