LHRC yaishika pabaya Dowans

LHRC yaishika pabaya Dowans

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
LHRC yaishika pabaya Dowans

Monday, 31 January 2011 19:44 newsroom



* Yaenda kortini kuzuia malipo ya bilioni 94/-
NA MWANDISHI WETU
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimewasilisha pingamizi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kupinga usajili wa tuzo iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC). ICC ilitoa tuzo kwa kampuni ya Dowans, ikiliamuru Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuilipa Dowans sh. bilioni 94.
LHRC iliwasilisha pingamizi hilo jana, baada ya Mahakama Kuu kupokea maombi ya Dowans ya kutaka kusajiliwa kwa tuzo hiyo.
Maombi hayo ya madai namba 8 ya mwaka huu, yalifunguliwa na Dowans Holdings S.A na Dowans Tanzania Limited dhidi ya TANESCO.
Dowans iliwasilisha maombi hayo mahakamani Januari 25, mwaka huu, kupitia kampuni ya uwakili ya nchini ya Kennedy Fungamtama.
Kiongozi wa jopo la mawakili lililofungua pingamizi dhidi ya tuzo ya ICC kwa Dowans, Dk. Sengondo Mvungi, alisema liliwasilishwa jana mchana, hivyo wanasubiri kuitwa mbele ya jaji atakayepangiwa kulisikiliza.
Dk. Mvungi alisema wanapinga usajili wa tuzo hiyo kwa kuwa, kufanya hivyo ni utekelezaji wa malipo, kwani itakuwa hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, ambayo itapaswa kutekelezwa na vyombo vya haki.
Alisema wanapinga kusajiliwa tuzo hiyo, kwani imepatikana kwa siri, ilikuwa na hila na haikupatikana kwa mujibu wa taratibu za kisheria.
Dk. Mvungi alisema pia haifungamani na sheria za Tanzania na haikuzingatia sera za nchi, hivyo haistahili kuitwa tuzo.
Novemba 15, mwaka jana, ICC ilitoa tuzo kwa Dowans na kuitaka TANESCO kuilipa kampuni hiyo ya kufua umeme wa gesi fidia ya sh. bilioni 94, uamuzi ambao umekuwa ukipingwa na wananchi na baadhi ya wanaharakati.
Kampuni ya Dowans iliomba ilipwe dola milioni 149 na TANESCO kwa kuvunja mkataba wa kuzalisha megawati 100 za umeme.
Dowans ilirithi mitambo ya Kampuni ya Richmond, ambayo ilipewa zabuni ya kufua umeme wa dharura kutokana na nchi kukumbwa na matatizo ya nishati hiyo mwanzoni mwa mwaka 2006. Richmond iliingia mkataba wa kuzalisha megawati 100 kila siku.
 
Unapona gazeti linalomilikiwa na CCM yaani Uhuru linaiandika habari hii ujue basi ipo kazi kwa mafisadi wote ambao wanachochea mafiga ya DOWANS...........................kwa minajili yao kulipora taifa hili kwa mradi wao binafsi............................
 
Back
Top Bottom