LHRC yalaani mauaji ya Katibu wa CCM mkoani Iringa Christina Kibiki, yatoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa haraka

LHRC yalaani mauaji ya Katibu wa CCM mkoani Iringa Christina Kibiki, yatoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa haraka

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Siku ya leo Novemba 13, 2024 Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa tamko kufuatia kifo cha Christina Kibiki, aliyekuwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa.

Mapema siku ya leo Christina Kibiki aliripotiwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake kijijini Njia Panda ya Tosa na alifariki dunia baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Tosamaganga mnamo usiku wa Jumanne, Novemba 12.

TL1.jpg


TL2.jpg

Soma pia: aribio la Utekaji wa Deogratius Tarimo: LHRC yahimiza uchunguzi wa haraka, jamii kutimiza wajibu wa kulinda uhai kila mtu

Kupitia tamko lao la hivi karibuni LHRC imelaani vikali mauaji hayo, yakisema ni mwendelezo wa matukio ya kihalifu yanayofanywa na watu wasiojulikana, jambo linalotishia usalama wa raia na kisha wametoa wito kwa Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa haraka ili kuwabaini na kuwafikisha wahusika mahakamani.

Aidha taasisi hiyo imehimiza vyombo vya usalama kuimarisha juhudi za kudhibiti matukio ya kihalifu na kushirikiana zaidi na jamii katika ufuatiliaji wa wahusika wa matukio haya.
 
Back
Top Bottom