Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania (LHRC) kimelaani kikali kitendo cha kikatili alichafanyiwa Edger Mwakalebela maarufu kama Sativa.
Iliripotiwa kwamba, baada ya kutekwa, aliteswa na kushambuliwa kikatili kabla ya kupatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi siku ya tarehe 27/06/2024 akiwa na majeraha makubwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
LHRC imelaani vikali tukio hili kwani matukio kama haya sio tu yanapoka Haki za Binadamu na kutweza utu lakini pia yanaashiria hali ya hatari na udhaifu wa usalama wa raia.
LHRC inalaani vikali tukio la utekaji na kushambuliwa kwa Bwana Edgar na matukio yote kama haya kwa kuwa ni ukiukwaji wa moja kwa moja wa Haki za Binadamu zilivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ikiwemo;
Ibara 13 (6) (e) inayoweka katazo dhidi ya mateso, ukatili, na adhabu za kinyama, Ibara ya 14 inayoainisha haki ya kuishi, Ibara ya 15 inaweka haki ya usalama wa mtu binafsi na ulinzi dhidi ya vurugu sambamba na haki ya uhuru na usalama wa mtu kutokukamatwa na kuwekwa kizuizini kinyume na sheria za nchi.
LHRC inatoa wito kwa mamlaka husika;
1. Kufanya uchunguzi wa haraka na wa kina kuhusu utekaji nyara na shambulio dhidi ya Edgar Mwakabela.
2. Kuhakikisha wale waliohusika na matendo haya ya kikatili wanakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.
3. Kutoa huduma za matibabu na msaada wa haraka kwa Edgar Mwakabela ili kusaidia afya yake kutoka kwa maumivu ya kimwili na kisaikolojia aliyopitia.
4. Kuchukua hatua za mahususi kuweka ulinzi wa ziada wa Bwana Edgar dhidi ya kitendo hicho kujirudia.
Soma zaidi ====>> SATIVA: Nilitekwa nikapelekwa Karakana ya Polisi Oysterbay kabla ya kusafirishwa sehemu nyingine na nimepigwa risasi ya kichwa