Library ya NBAA ovyooo kabisa !

Joined
Aug 10, 2011
Posts
35
Reaction score
13
Nilishangaa nilipoingia kwenye Library ya NBAA na kukuta ma-shelve ya kuhifadhia mikoba yametolewa nje halafu kuna tangazo kwamba”Weka mkoba wako hapa lakini uulinde mwenyewe. Kitu chochote kikipotea NBAA haitohusika”

Niliweka mkoba wangu na kwenda kujisomea. Lakini nikaanza kujiuliza hivi hawa jamaa wa NBAA wapo sawa kweli ?Kwa maana tangu nianze kusoma Chekechea sijawahi kuona unaingia library halafu mkoba unauacha nje bila ya kuwa na mtu wa kuutizama kwa utaratibu maalum.Halafu eti ukae na kujisomea kwa amani bila ya kuwa na wasiwasi wa begi lako.

Kwa sisi tunaojua nini maana ya Library tunajua kabisa hatujatendewa haki. Kwa sababu utaratibu huu unafanya wanafunzi wajisomee huku wakiwa na wasiwasi na mikoba yao.Hivi huyu mwanafunzi ataelewa kweli ? Halafu huu utaratibu ni maalumu kwa library hii tu ya NBAA ? kwa maana hatujauona kwenye Library zingine. Waturuhusu basi kuingia na mabegi yetu, si wameweka mlinzi wa kupekua kila mtu akitoka.

Ndio maana nasemaga kwamba ni bora kuwe na NBAA hata tano hapa nchini kwetu.Si unajua tena wanaringa kwa kuwa wapo wenyewe tu nchi nzima kama Tanesco. Kwa kweli kitendo cha kuanza utaratibu wa kuweka mabegi nje bila ya mtu wa kuyachunga ni dharau kubwa sana kwa wanachama wa NBAA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…