Licha ya Historia iliyotukuka, Kilwa imesahaulika, imechoka

Licha ya Historia iliyotukuka, Kilwa imesahaulika, imechoka

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
WIKI iliyopita nilielezea habari za vivutio vya utalii ambavyo havitangazwi na kwa kweli havitunzwi kabisa kwani hakuna miundo mbinu iliyowekwa ili vifikike kwa urahisi na watalii wa ndani.

Mmoja wa wasomaji aliniandikia kutaka kujua kwa undani habari za Washiraz na jinsi walivyoweza kuathiri mila na historia yetu, na hasa maeneo ya pwani, na alitaka kujua zaidi kuhusu hapo Kilwa Kisiwani.

Kwa ufupi Washiraz sio Waarabu, wao ni watu wa asili ya Aryans na kwao kwa asili ni Shiraz, moja ya jimbo mashuhuri kusini mwa Iran.
Haijulikani sababu ya kuondoka na kuja, huku iingawa taarifa mkanganyiko zinasema njaa na ukame vilifanya Washiraz waliokuja pande hizi kuhama kutafuta maeneo ya kukaa na tufani la baharini likawamega wakapoteana na wengine wakajikuta wamefika huku.

Ingawa ushahidi kuhusu hilo haupo kwani unaona kabisa kuwa wale waliokuja huku, kwa uchambuzi wa ustaarabu, ujenzi na shughuli walizozifanya, wanaonekana ni watu waliodhamiria kuhamia mbali na kwao na sio kuwa walifika huku kwa bahati mbaya.

Washirazi ndio waliouanzisha mji wa Zanzibar. Zanz- bar- kwa maana ya mji wa watu weusi. Na kuna miji kama Mikindani na Mafia bado ina athari ikiwa pamoja na kuendelea kuwepo kwa kizazi chao kilichochanganyika na Waswahili.

Kilwa Kisiwani ndio yalikuwa makao makuu yao ya kiutawala na kibiashara pia yakiunganisha biashara za pembe na madini ya dhahabu hadi Msumbiji, Zimbabwe na Malawi.

Lakini makazi yao pale Kaole, Bagamoyo yanaonyesha ushahidi kuwa walikuwa wakifanya biashara na watu wa mashariki ya mbali hasa China na Japan.

Ujenzi unaonyesha kuwa walikuwa wamekwisha staarabika kwa kiasi kubwa kwa kuwa na majumba ya kifahari na yenye huduma za mabwawa ya kuogelea na vyoo vya ndani.

Utaona kuwa kuna kufanana sana kwa aina ya ujenzi wa Msikiti Mkuu wa pale Kilwa Kisiwani na baadhi ya misikiti ya kale sana huko Shiraz.

Jengo la makao makuu ya Sultan bin Sulaiman pale Kilwa Kisiwani ( Husun Kubwa) lilikuwa na kila aina ya ufahari kwa kiwango cha wakati ule. Bafu la ndani, bwala ka kuogelea na vyumba vya mikutano na vya kulala.

Licha ya kuwa na ikulu yake alikuwa na ngome yake. Na kule kwenye ngome yake, kiasi cha nusu kilomita kutoka ikulu, palikuwa na nyumba yake nyingine iliyokuwa na choo cha ndani na mfumo wa majitaka wa namna hiyo ambayo hadi leo unatumika.

Kwa pande hizi za Afrika Mashariki na huenda kwa nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara, hizo zilikuwa ndio nyumba za kwanza zenye bwawa la kuogelea na choo cha ndani kwa ndani.

Kilwa Kisiwani kilikuwa ndio kitovu cha kueneza dini ya Uislamu na kwa kweli kuna historia ndefu ya magwiji wa elimu ya dini na mashehe walitokea pande zile na hadi leo eneo kama Kilwa Pande bado hutumika kama kituo cha imani na kila mwaka hufanyika ibada maalumu inayokusanya waumini kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Washirazi walianzisha pia mji wa Kilwa Kivinje na kuifanya bandari kuu ikiunganisha visiwa vya Comoro, Shelisheli, Mafia, Unguja na Pemba, Mombasa na hadi leo safari hizo zinaendelea kufanyika.

Kilwa Kivinje, ambako ndiko kuna hospitali ya Wilaya ya Kilwa ya Kinyonga (eneo ambalo Wajerumani waliwanyonga wapinzani wa vita vya Majimaji) , paliwahi kuwa makao makuu ya eneo lile kabla ya kuhamia Kilwa Masoko.

Licha ya kuwa na historia iliyotukuka namna hiyo, ukifika Kilwa Kisiwani utakachokutana nacho ni misitu na makazi duni ya watu wachache sana wanaoishi kule. Sasa hivi ni hifadhi ya kihistoria chini ya idara ya mambo ya kale.

Credit: Charles Kayoka
 
Pande, kukiogopeka sana kwa sayansi giza, kama umewahi kuishi Kilwa utakuwa na habari hii.
 
Back
Top Bottom