Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tunaona kwenye ripoti mbalimbali za fedha za Kila mwaka za CAG, zikiibua ufisadi mkubwa wa mabilioni, unaofanywa na watendaji Serikalini, lakini tunaona ni "business as usual" inayoendelea na hakuna hatua zozote za kuwafikisha watuhumiwa kwenye vyombo vya Sheria zinazochukuliwa!
Tunashuhudia Polisi wa nchi yetu, wakituhumiwa Kwa makosa mbalimbali, yakiwemo ya mauaji jwa mahabusu kwenye vituo vya Polisi, lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa za kuwawajibisha watendaji hao!
Nimekuwa nikijiuliza, hivi haya magereza yetu yana watu wa "class" fulani pekee, ambao ndiyo wanastahili kwenda huko na baadhi ya watu wa nchi hii Wana "impunity" ya kutoshitakiwa?
Tunajua pia kuwa magereza yetu, yamejaza wafungwa wengi wa makosa madogo madogo kama vile wezi wa simu za mkononi, lakini ni nadra Sana kumkuta kigogo aliyeiba mabilioni ya shilingi za watanzania,, akiwa amefungwa huko magerezani!
Hivi tuseme Kwa kuwa nafasi nyingi ni za kuteuliwa na Mheshimiwa Rais, ndiyo inawatengenezea Kinga ya kutoshitakiwa, wateule hao?
Watanzania tunaumizwa Sana na gharama za maisha, ambapo Kila kukicha bei za bidhaa mbalimbali zinapanda.
Vile vile nchi hii ni Moja ya nchi ambayo inawatoza Kodi nyingi wananchi wake, ambapo badala ya pesa hizo kwenda kwenye shughuli za maendeleo, zinaishia kwenye mifuko ya watendaji wachache wa Serikali.
Kwa hiyo baadhi ya watendaji Serikalini, wanachojua ni "Kula Kwa urefu wa kamba zao" hadi wanavimbiwa!
Kama Rais wetu, kweli una nia safi ya kulijenga Taifa hili Kwa usawa, bila kumwangalia usoni mtendaji, basi Taifa linakutegemea wewe uweze kuwatumbua, watendaji wote wa Serikali, wenye kutuhumiwa na wizi wa mabilioni ya pesa za walipa Kodi wa nchi hii.
Mungu ibariki Tanzania