Licha ya Mogogoro hii, Yanga SC itakuwa Bingwa wa Ligi msimu 2016/17.

lil wayne

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2016
Posts
992
Reaction score
904
Kumejitokeza machache sana hapa katikati, baadhi ya hayo yanaonekana na kusemekana kuwa yataiyumbisha sana Dar es Salaam Young Africans SC hadi ishindwe kufanya vyema kwenye msimu wa mwaka 2016/17.

Nipende kuwakumbusha na kuwataarifu tu kuwa kitu pekee ambacho kinachoweza kuiyumbusha Yanga International ni wachezaji kukosa kulipwa mishahara na marupurupu yao. Vinginevyo sioni sababu itakayo fanya wachezaji hawa washindwe kutembeza dozi kama iliyotembezwa msimu uliopita.

Nadhani ndani ya mioyo yenu mnatambua kuwa ubora(performance) ya watu kama Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Juma Abdul, Kelvin Yondani, Saimon Msuva, Nadir Haroub haiwezi kuathiriwa na kinachoendelea klabuni, na hii ni kutokana na jinsi ambavyo Yanga ilivyo sasa ambapo kuteteleka kwa aina yeyote ile kwa Utawala hauwezi kuathiri utendaji wa wachezaji.

Hili limethibitika leo, kila mtu ameona ubora wa kikosi cha mseto cha Yanga ambacho kimesheheni wachezaji wa kikosi cha ziada, na wengine kucheza nafasi zisizo zao kutokana na kuwa na wachezaji 5 wa first 11 kuwa majeruhi.

licha ya kuwa tumeshindwa kumaliza mchezo ndani ya dakika 90. Napenda kuwahakikishia kuwa mpaka sasa nimelithibitisha kuwa hakutakuwa na mpinzani wa kuogopeka kwenye LIGIKUU ambaye ataweza kuhandle mikikimikiki ya Ligi kama Yanga.

Yanga SC itakuwa Bingwa tena na kwa mara nyingine mfululizo msimu huu 2016/17.
 
Endelea kuota huku unatembea Kamusoko atakuwa Sokomoko na Twite atakuwa Twire...Leo Niyonzima kasema oooh jamani Bocco ndo michezo gani hiyo...Azam tumekuja kuwashika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…