Licha ya watani(yanga) kuchezea kichapo, huu mkwanja unawahusu

Licha ya watani(yanga) kuchezea kichapo, huu mkwanja unawahusu

lil wayne

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2016
Posts
992
Reaction score
904
Licha ya ndoto za watani wangu Yanga SC kutinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kufifia, inaonekana hawata rudi bure.

Hatua ya Makundi #CAFCC atakayemaliza

4th gets $150k (327,820,968Tsh).
3rd gets $240k (524,518,709.Tsh).

Huu mkwanja ni sawa na udhamini wa Azam kwa misimu 3.

Hapa tuna la kujifunza na sisi kama Simba SC, Tunawaasa viongozi kuwa msimu ujao tunahitaji kushiriki kama sio klabu bingwa then iwe Shirikisho..... Mbwembwe na visingizio vya kijinga pale tunapo fanya ovyo kwenye Ligi vifikie ukomo msimu 2016/17.
 
Wanahabari wetu sijui mtaripoti vipi..!
sijui mtakuja ni ile ile 'kafa kiume'?Kandanda letu lipo mdomoni na kwenye magazeti....!huwa hatuumizi kichwa kutafuta tatizo lipo wapi?
Sawa tumefungwa.... Lakini ni kheri sie tulio fungwa lakini tunabeba mamilioni...
Kuliko wewe unayeshinda mechi za kirafiki wala hupati hata cent.
 
Sawa tumefungwa.... Lakini ni kheri sie tulio fungwa lakini tunabeba mamilioni...
Kuliko wewe unayeshinda mechi za kirafiki wala hupati hata cent.
Ukishaweka mamilioni kibindoni unatulia..!unasubiri mwakani wala hutaki kujiuliza kosa liko wapi?hapo ndipo ilipolala hoja kuu ..! Tunampataje bingwa wetu!Ligi yetu ikoje?Marefarii wako fair?Badala ya kuwajaza misifa wachezaji,timu kiujumla udhaifu uko wapi?Kwa Yanga hii 1 mpaka 5 kunahitajika marekebisho makubwa(japo wapo watakaosema kipa kaokoa penati).
 
1469567637902.jpg
 
Licha ya ndoto za watani wangu Yanga SC kutinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kufifia, inaonekana hawata rudi bure.

Hatua ya Makundi #CAFCC atakayemaliza

4th gets $150k (327,820,968Tsh).
3rd gets $240k (524,518,709.Tsh).

Huu mkwanja ni sawa na udhamini wa Azam kwa misimu 3.

Hapa tuna la kujifunza na sisi kama Simba SC, Tunawaasa viongozi kuwa msimu ujao tunahitaji kushiriki kama sio klabu bingwa then iwe Shirikisho..... Mbwembwe na visingizio vya kijinga pale tunapo fanya ovyo kwenye Ligi vifikie ukomo msimu 2016/17.

Sisi hatuhitaji sana huo mchanganuo wako wa fedha bali tunataka mafanikio ya kimpira kwa Klabu ya Yanga kwani tunachukizwa kila mara wao kuishia raundi hizi hizi za mapema. Tuache kufarijiana " kinafiki " please. Mafanikio ya Uwanjani yana heshima sana kwa Klabu na nchi kuliko hizo fedha. Yanga imefungwa period tusije tena na analysis za kipuuzi kama hizi.
 
Siyo upuuzi
Wamefika robo fainali kwa mara ya kwanza tangu miaka ya tisini

Na kwa mara ya kwanza kwa klabu yyte ya tanzania tangu mwaka 2003, ndio wametoka ila hawajotka hivi hvi lazima tu ackonwldge hilo

Sidhani kama kuna upuuzi hapo
 
Hata hivyo, nafasi ya nne itapimwa baada ya timu 2 kutoka kila kundi. Jamaa yaani hadi huruma. Fukuzeni mabeki wote wazee.
 
Ajenda ya fedha ilijulikana hata kabla hawajacheza mechi ya kwanza ktk robo fainfali. Sasa hivi current news ni matokeo kwanza
 
Siyo upuuzi
Wamefika robo fainali kwa mara ya kwanza tangu miaka ya tisini

Na kwa mara ya kwanza kwa klabu yyte ya tanzania tangu mwaka 2003, ndio wametoka ila hawajotka hivi hvi lazima tu ackonwldge hilo

Sidhani kama kuna upuuzi hapo

Ukisema kuwa Yanga wamefikia mafanikio tangu 2003 halafu hapo hapo umesahau kuwa Simba ilifikia mafanikio makubwa zaidi ya hayo mwaka 1993 kidogo napatwa na wasiwasi wa aina ya uelewa na ufuatiliaji wako mzima wa masuala ya Soka hapa nchini Tanzania. Naomba kusisitize kuwa penda mno kufanya tafiti kwanza ndipo uje humu na data za uhakika. Kuna mafanikio gani ya CAF ambayo Yanga imeyafikia Simba hajayafikia? Labda rekodi ambayo Yanga imeizidi Simba ni hii ya kila mara wao kushiriki katika mashindano haya lakini hatuoni tija na mafanikio yao na badala yake wanatolewa mapema mashindanoni kila mara. Kwa hili lazima nikiri kuwa Yanga wametushinda Wana Simba na labda niwapongeze pia.
 
Wanahabari wetu sijui mtaripoti vipi..!
sijui mtakuja ni ile ile 'kafa kiume'?Kandanda letu lipo mdomoni na kwenye magazeti....!huwa hatuumizi kichwa kutafuta tatizo lipo wapi?
Jamani, ni kuzidiana viwango tu. Hata Euro na World cup wanakuwepo wa mwisho kwenye makundi. Cha msingi ni timu zetu kupambana zijiimarishe ili viwango vyake viwe na uwezo wa kushindana na timu za nje. Kwa Simba SC ambayo kwa muda imeshindwa kabisa kupata nafasi za uwakilishi japo ni giant ktk soka la Tanzania, wanatakiwa kushughulikia changamoto hii. Naona mentality yao imekuwa ya ku-assume kwamba kwa kuwa Yanga inaelekea kushindwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo, basi ni mbovu kuliko Simba. Ikiendelea hivyo, wataendelea kuwa watazamaji na washangiliaji wa timu za kigeni.

Kila timu inatakiwa kubadilika.
 
Ni kweli kwamba hatujafanya vema shirikisho, lakini ni faida nyingi sana zinapatikana tofauti na aliye milimani akifanya mazoezi: Yanga wananufaika na exposure ya wachezaji, uzoefu Wa mechi za kimataifa, kukuza uchumi wao; Uhakika ni kuwa licha ya matokeo mabaya ila Wamepata funzo kubwa, sidhani next time hawa tajipanga !!! Kwa timu ile na level ya mashindano, timu za ligi kuu yetu zitapigwa sana!!
 
Ukisema kuwa Yanga wamefikia mafanikio tangu 2003 halafu hapo hapo umesahau kuwa Simba ilifikia mafanikio makubwa zaidi ya hayo mwaka 1993 kidogo napatwa na wasiwasi wa aina ya uelewa na ufuatiliaji wako mzima wa masuala ya Soka hapa nchini Tanzania. Naomba kusisitize kuwa penda mno kufanya tafiti kwanza ndipo uje humu na data za uhakika. Kuna mafanikio gani ya CAF ambayo Yanga imeyafikia Simba hajayafikia? Labda rekodi ambayo Yanga imeizidi Simba ni hii ya kila mara wao kushiriki katika mashindano haya lakini hatuoni tija na mafanikio yao na badala yake wanatolewa mapema mashindanoni kila mara. Kwa hili lazima nikiri kuwa Yanga wametushinda Wana Simba na labda niwapongeze pia.
Nakubali Simba wame wahi kufanya vizuri zaid ya Yanga lakin nasema wame toka pia kwa sababu ya kukosa uzoefu wa hatua kama hizi ki ma shindano
Simba huwa wana fanya vzuri kuliko yanga waki ingia CAF, lakin hatuna budi kusema hata hapo Yanga walipo fika si mbaya
Na zawad walo ipata si haba
 
Unajua maana ya pongezi na labda inavyotakiwa kutolewa kwa kumaanisha? Yanga ingepongezwa kama unavyotaka endapo basi hata mechi zake kadhaa tu za michuano hii ya Shirikisho ingeshinda angalau mechi moja au mbili au ivuke lakini kusema kuwa eti Yanga inatakiwa tuipongeze kwa hatua iliyofikia labda " wapuuzi " wasiojua mpira watakuunga mkono ila kwa " wachambuzi " tuliobobea hapo tunasema " work done zero ". Na Watu wa aina yako ndiyo mnayoiponza Yanga kwa kuipa sifa ambazo kimsingi hawana na matokeo yake wakienda nje tu ya Tanzania " wanachezea " tu vipondo. Jifunze sana kufanya analysis hasa ya mpira. Mimi ni Simba damu nadhani hakuna asiyenijua humu ila napenda kuzungumza mpira na siyo ushabiki. Muda wowote nitakuja na analysis yangu ya kuihusu Timu yangu ya Simba ambayo ukiisoma utajifunza vitu vingi. Yanga bado wana safari ndefu mno ila Simba tuna mtihani mgumu sana wa kufanikiwa kimpira lakini Azam naona wanachezea tu Shilingi chooni ambayo siku ikitumbukia watakuja kujuta.
 
Back
Top Bottom