licorice root ni nini

fundibenz

Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
61
Reaction score
67
Samahani,nimeona kwenye mtandao mizizi ya licorice ni tiba,sasa nauliza kwa kiswahili ni nini..na naweza nikaipataje?
 
Samahani,nimeona kwenye mtandao mizizi ya licorice ni tiba,sasa nauliza kwa kiswahili ni nini..na naweza nikaipataje?
Mkuu licorice root ni dawa ya kiarabu na wahindi pia wanayo ni dawa ya kutibu maradhi mengi mwilini. Kwa kiswahili licorice root ni Mizizi ya Arkisusi kama upo mjini Dares-Salaam nenda maeneo ya karibu ya Soko kuu la Kariakoo mtaa wa mkunguni na nyamwezi kuna wanaouza dawa za kiarabu aka Dawa za kisuna ulizahiyo dawa Arkisusi aka (licorice root) angalia nitaiweka ahpo pichani kw achini utaweza kuipata .Mimipia katika dawa zangu huwa ninaitumia sana kutibu maradhi mengi tu. ninakuwekea baadhi ya amtibabu yanayotibiw ana hiyo dawa ya licorice root aka Arkisusi

GESI TUMBONI (COLIC): Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo.

TIBA: Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni.


 

Nashukuru sana kwa maelezo mazuri tena ya kina,nimesoma kuwa ukichanganya licorice na asali na mdalasini kwa pamoja ni dawa ya kusaidia kupunguza kukoroma,je ni kweli na unaufahamu mchanganyiko huu,asante
 
Nashukuru sana kwa maelezo mazuri tena ya kina,nimesoma kuwa ukichanganya licorice na asali na mdalasini kwa pamoja ni dawa ya kusaidia kupunguza kukoroma,je ni kweli na unaufahamu mchanganyiko huu,asante
Mimi hiyo dawa uliyoeleza sijuwi .Dawa ya kukoroma Fanya hivi: Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20. Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma
na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu. Tumia hiyo dawa yangu kisha uje hapa utupe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…