Lifahamu Daraja la Ruaha Mkuu - Morogoro

Lifahamu Daraja la Ruaha Mkuu - Morogoro

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

LIFAHAMU DARAJA LA RUAHA MKUU - MOROGORO

Muonekano wa Daraja la Ruaha Mkuu lenye urefu wa mita 133 katika barabara ya Mikumi- Kidatu - Ifakara sehemu ya Kidatu - Ifakara kilometa 66.9 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Morogoro.

Daraja hilo limejengwa na Mkandarasi Reynolds Construction Company - RCC ya Nigeria na Mhandisi Mshauri kutoka Kitengo cha Uhandisi (TANROADS Engineering Consulting Unit - TECU).

Usanifu na maandalizi ya nyaraka za zabuni ulifanywa na Kampuni ya kihandisi ya Crown-Tech Ltd ya Tanzania.

Ujenzi wa Daraja la Ruaha Mkuu limejengwa sambamba na barabara ya Kidatu - Ifakara kwa kiwango cha lami, Ujenzi ulianza 02 Oktoba 2017 na kukamilika 30 Juni, 2024 kwa gharama ya Shilingi Billion 157.15, ikihusisha ujenzi wa barabara, daraja, usimamizi na fidia ya mali zilizoathiriwa na mradi.

Barabara ya Kidatu - Ifakara na Daraja la Ruaha Mkuu imefunguliwa rasmi leo Agosti 04, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.21.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.21.jpeg
    667 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.21(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.21(1).jpeg
    678.6 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.22.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.22.jpeg
    735 KB · Views: 11
  • WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.23.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.23.jpeg
    908.8 KB · Views: 10
  • WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.23(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.23(1).jpeg
    841.9 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.24.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.24.jpeg
    841.1 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.25.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.25.jpeg
    891.5 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.27.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.27.jpeg
    851.7 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.28.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.28.jpeg
    890.2 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.28(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-04 at 14.32.28(1).jpeg
    882.2 KB · Views: 8
Sawa Tumeona Kodi Zetu Na Mchango Mkubwa Wa Mabeberu Yaani Mikopo
 
LIFAHAMU DARAJA LA RUAHA MKUU - MOROGORO

Muonekano wa Daraja la Ruaha Mkuu lenye urefu wa mita 133 katika barabara ya Mikumi- Kidatu - Ifakara sehemu ya Kidatu - Ifakara kilometa 66.9 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Morogoro.

Daraja hilo limejengwa na Mkandarasi Reynolds Construction Company - RCC ya Nigeria na Mhandisi Mshauri kutoka Kitengo cha Uhandisi (TANROADS Engineering Consulting Unit - TECU).

Usanifu na maandalizi ya nyaraka za zabuni ulifanywa na Kampuni ya kihandisi ya Crown-Tech Ltd ya Tanzania.

Ujenzi wa Daraja la Ruaha Mkuu limejengwa sambamba na barabara ya Kidatu - Ifakara kwa kiwango cha lami, Ujenzi ulianza 02 Oktoba 2017 na kukamilika 30 Juni, 2024 kwa gharama ya Shilingi Billion 157.15, ikihusisha ujenzi wa barabara, daraja, usimamizi na fidia ya mali zilizoathiriwa na mradi.

Barabara ya Kidatu - Ifakara na Daraja la Ruaha Mkuu imefunguliwa rasmi leo Agosti 04, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mbona liko chini sana? Mvua za maana hazitapita nalo? Wangelinyanyua kama pale Ruvu
 
Mbona daraja liko chini sana, hapo mvua ya maana ikipiga naona maji yanapita juu ya daraja. Anyway inawezekana ni macho yangu pia
 
Asante kodi yangu

Kazi ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom