Lifahamu jiwe la Moabu(MOABITE STONE)

Lifahamu jiwe la Moabu(MOABITE STONE)

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
Moabu , "Mbegu ya baba"; ni jina la kihistoria la eneo la milimani upande wa mashariki wa Bahari ya Chumvi ndani ya nchi ya kisasa ya Yordani. Ilikuwako kati ya Edomu upande wa kusini na Amoni upande wa kaskazini.

Zamani eneo hilo lilikuwa ufalme wa Wamoabu. Mji wake mkuu uliitwa Diboni na maghofu yake yapo karibu na mji wa Dhiban wa kisasa.


Sawa na Isreli Moabu ilikuja chini ya mamlaka kwanza ya Ashuru na baadaye ya milki ya Babeli. Mwaka 582 KK mfalme Nebukadnezzar II wa Babeli alifanya Moabu kuwa sehemu ya milki yake; hivyo ilikuwa sehemu ya ufalme wa Uajemi baadaye. Wakati wa utawala wa Kiajemi Moabu ilipotea kama taifa la pekee. Makabila ya Waarabu walianza kuingia na kukalia sehemu kubwa za nchi na wakazi waliacha lugha yao wakatumia Kiaramu badala ya lugha yao ya awali


Jiwe la Moabu

katika mwaka wa 1868 kule Diboni, Yordani Kulipatikana jiwe lifaamikalo kama MOABITE STONE lililogunduliwa na mwana akiolojia na mmishionari wa ujerumani Klein,

Jiwe hili linathibitisha vita ya wa moabu dhidi ya Israeli kama ilivyoandikwa katika 2Fal 2 na 3.

Kati ya shuhuda za kiakiolojia za kabila hili la wa moabu ni Jiwe la Mesha, linaloeleza ushindi wao dhidi ya mwana wa mfalme Omri wa Israeli.

1619285584601.png

JIWE HILI LILIKUTWA LIMEANDIKWA MANENO HAYA

“Mimi ni Mesha […] mfalme wa moabub […] Omri alikuwa mfalme wa Israeli, na akawatesa moabu Moabu […]Nilichukua kutoka humo vyombo vya Yehova […] ilihali nyumba ya Daudi ilimiliki Horonaimu


Jiwe la moabu ni maelezo ya matukio yanayofanana na 2 Wafalme sura ya 3. Watu kadhaa wa bibilia na mahali hutajwa:

1619285427570.png


1619285475248.png


Jiwe la MOABU Lilikuwa na umri unaokaribia miaka 3,000. Ni kipande cha jiwe la basalti jeusi lililosuguliwa likiwa na upande wa juu ulioviringishwa vizuri, lilikuwa na kimo cha karibu meta 1.2 likipita kidogo tu upana wa meta 0.6, na likiwa na unene unaokaribia meta 0.6.

1619284992238.png


1619285017839.png


1619285346368.png
 
So what? linaabudiwa au ni sawa tu Takataka za kale?
 
Nauliza hiyo ardhi unayoikanyaga hapo kwako ina umri gani?
 
Nini baada ya hilo jiwe kinafuta out of history..?
 
Back
Top Bottom