Son of the universe
New Member
- May 29, 2024
- 3
- 6
Ndugu zangu naamini nanyi mnakerwa sana na jinsi fedha za walipa kodi zinavyotumika vibaya kupitia ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, majengo ya shule, soko, hospitali na mengineyo chini ya kiwango.
Jambo hili limekuwa sio tu likipoteza fedha nyingi za walipa kodi lakini pia likihatarisha uhai na usalama wa watumiaji wa miundombinu hiyo. Tunashuhudia ajali nyingi za barabarani zinazosababishwa na ubovu wa barabara hizo. Watu wengi wamekufa na mali nyingi kuharibika kwa kusombwa na madaraja. Majengo yamekuwa yakiporomoka na kuua watu na kuharibu mali nyingj kwa sababu ya kujengwa chini ya viwango.
Miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikitajwa ni pamoja na rushwa zinazotolewa katika uchukuaji wa zabuni hizo za ujenzi na hivyo kupelekea kupewa wakandarasi wasio na sifa na vigezo vya kufanya kazi hizo. Pia uzembe na usimamizi mbovu wa watendaji wa serikali wanaopewa kazi za kusimamia miradi hiyo.
Ujenzi huu wa chini ya kiwango pia umekuwa ukisababisha uchelewaji wa kukamilika kwa miradi husika pamoja na kudumu kwa muda mfupi zaidi tofauti na matarajio yake na hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa fedha zinazotumika kujenga upya miradi hiyo.
NINI KIFANYIKE?
Kama nchi tumekuwa na utaratibu wa kuita miundombinu hiyo majina ya viongozi au watu waliotoa mchango fulani katika jamii na taifa kwa ujumla. Mfano barabara ya Nyerere, Daraja la Kikwete, Hospitali ya Benjamin Mkapa na mengine mengi ya aina hiyo ikiwa kama sehemu ya kuenzi michango ya watu hao katika maendeleo ya taifa letu.
Napendekeza maboresho kidogo katika utaratibu huu kwa kuongeza na majina ya mkandarasi aliyehusika katika ujenzi huo pamoja na muda aliotumia kukamilisha mradi husika.
Mfano: Barabara ya Mandela, imejengwa na kampuni X kwa muda wa miaka 5.
Faida itakanayo na maboresho haya ni pamoja na kuongezeka kwa viwango na ubora katika miundombinu husika kwa sababu makndarasi atajua kuwa mapungufu yoyote yatakayoonekana katika mradi husika basi yatamharibia soko na uwezekano wa yeye kupatiwa miradi mingine kama hiyo. Na wakati huo huo ubora utakaoonekana katika mradi husika utasaidia kumtangaza zaidi kibiashara na hivyo kumuongezea faida zaidi na kuzidi kumpa hamasa ya kuendelea kujenga kwa ufanisi na ubora zaidi.
Hivyo hivyo muda uliotumika katika ujenzi wa mradi utaonesha kama anakamilisha miradi kwa wakati na hivyo apewe miradi mingi zaidi au anachelewesha miradi na hivyo kunyimwa miradi mingine zaidi.
Ni matumaini yangu kuwa utaratibu huu utaongeza umakini na ufanisi zaidi miongoni mwa wakandarasi na hata viongozi na watendaji wanaowapa wakandarasi hao zabuni za ujenzi wa hiyo miundombinu kwa sababu inawafichua wazi kwa jamii ili iweze kuwajua na kuwatambua na matokeo ya kazi zao.
Kwa utaratibu unaotumika sasa wa kuita majina ya viongozi pekee kwenye hiyo miundombinu bila uwepo wa majina ya kampuni za wakandarasi waliohusika kuijenga kunafanya wakandarasi hao waendelee kujificha bila kutambulika na hivyo kuendelea kulinda udhaifu wao katika ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu husika na hata kuendelea kulinda watendaji waliowakabidhi zabuni za ujenzi wa miundombinu hiyo.
Ziko barabara zina mashimo huku zikiwa bado mpya na zingine kabla hata hazijaanza kutumika lakini wakandarasi waliozijenga jamii haiwatambui na hivyo kuendelea kupewa zabuni mpya na kurudia mapungufu yale yale. Yako majengo yamepasuka kabla hata hayajaanza kutumika kwa sababu yamejengwa chini ya kiwango lakini mkandarasi wake hajulikani na anaendelea kujenga majengo mengine mapya
kila kukicha.
Zipo barabara zimejengwa kwa viwango vya hali ya juu sana hadi unatamani kujua zimejengwa na mkandarasi yupi, yapo pia majengo ya shule, hospitali, mahakama na masoko yamejengwa kwa viwango vya hali ya juu lakini wakandarasi wake hawatambuliwi na serikali, hivyo ni vyema sasa uanzishwe utaratibu wa kuwatambua kwa kuwaandika pamoja na majina ya viongozi wengine ili jamii iwatambue pia.
Jambo hili litasaidia kuboresha miundombinu yote inayoendelea kujengwa na mipya itakayoanza kujengwa nchi nzima hasa katika kipindi hiki ambacho ubovu wa miundombinu mingi umekuwa ukilalamikiwa zaidi.
Inawezekana wakati wa ujenzi mkandarasi asiwe makini zaidi kuzingatia ubora wa kazi anayoifanya lakini sidhani kama atavumilia kuona jina lake likiwa katika barabara yenye mashimo kuanzia mwanzo hadi mwisho na bado akarudia kufanya hivyo hivyo apewapo mradi mwingine.
Naiona Tanzania ambayo itakuwa na miundombinu bora zaidi inayozingatia viwango vya kimataifa pamoja uzalendo wa hali ya juu katika ujenzi wake kwa sababu tu inakwenda kuwatambua si tu viongozi pekee bali pia na wakandarasi waliopewa zabuni za kujenga miundombinu husika.
Tanzania yenye miundombinu bora na yenye viwango vya kimataifa na kisasa itawezekana kupitia kuwatambua wakandarasi pia kwa kuwaandika katika mbao za majina ya barabara na miundombinu husika.

Upvote
3