Life After Life: Je, wajua Magufuli huko alipo anayaona yote? Je, tuendeleze 'double standards' ya 'cherry picking' au tuiachie Karma iwashughulikie?

Una Uhuru wa kujieleza, lakini hiyo orodha yako na sababu za vifo vya ulio wataja una hakika navyo?
Au na wewe unazungumza kwa sababu umesikia "wakizungumza"?

NI kweli watajwa hawapo/hatuwaoni, iwe wamekufa, wametoweka, au vyovyote vile, haupaswi kuzungumza jambo usilo na ushahidi kamili, jifunze kuepuka kuzungumza kwa hisia!

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
Yaani post ni ndefu lakini yaliyomo ni uongo uongo mtupu. Mwongo sana wewe pasko. Mwongo kwa sababu Biblia yaliyo sauti ya Mungu unasema hivi katika Mhubiri 9:5-6:
5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
6 Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.

Ni mwongo zaidi wewe pasko unalosema watakaofufuliwa watakuwa na miili mipya sijui ya roho. Mwongo sana. Yani unapenda vijitu vya kishetani vya kutungatunga tu. Maandiko yanasema hivi katika 1Wakorintho 15:51-54
51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
Wacha uongo wako wa karma sijui ushetani gani wa mizimu. Yani uongo uongo tu.
Kwa hiyo huyo alipokuwa hajui chochote kinachoendelea na kama unataka kumtisha mtu usiendelee na huu uongo wa bei rahisi. Wacha uongo
 
Nini magufuri mitume na manabii pia walishatangulia mbele za haki atakuwa huyo dhalimu bhana muache sabaya anywe kikombe chake

Na wewe p usisahau kuwa ulimchongea mwandishi mwenzio wa habari mpaka kupelekea kifo cha mama yake

Na wewe unayo ya kujibu after life
 
Paskali leo umeleta mada dhaifu sana. Kwanza hayo mambo ya life after death ni dhana za kufikirika ambazo kwa msomi kama wewe ilitakiwa uwe unajua ni mambo yasiyoweza kuthibitishwa ambayo yanatakiwa kuaminiwa na laymen only.
areeviree hiyo makifo haikwepeki na kuna kunyooshwa huko hata tukijipa mahop vipi..
 
Nina uhakika nisemalo na sio lazima wewe ukubali.
 
Hapo kwenye double standard ulipashangilia sana wakati anayatenda mwendazake, leo ndio unaona Ni vibaya!

La zaidi hao wengi ingependeza kama ungewataja japo watatu tu ili kumsaidia SSH na watanzania kwa ujumla.
Unajua wakati mwingine akili za pasco huwa zinaenda likizo, andiko dhaifu lenye kutetea ujinga kabisa

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Kaka Paskali, ushaanza kuharibu, vp tena? Wajua hiyo hiyo kuwakamata na kuwafungulia mashtaka akina Sabaya ndio karma? Au una define vp karma? watu wanasubiri Makonda nae akamatwe, Mnyeti Alexander, yaani ile gang iliyokuwa ina ua watu ikamatwe wote na kufikishwa katika vyombo vya sheria.. Hiyo ndio karma. Mama yetu Samia, Rais wetu anafanya vizuri sana, watu wamejaa matumaini makubwa sana, sbb ana tenda haki kabisa, wacha walioua watu washughulikiwe kabisa
 
Paskali toa utopolo huu, yaani jamaa mmemwabudu hadi kufikia kuamini pamoja na kuwa amekufa lakini huko aliko bado anaweza kupiga chabo duniani?
 
Kaka Paskali, ushaanza kuharibu, vp tena? Wajua hiyo hiyo kuwakamata na kuwafungulia mashtaka akina Sabaya ndio karma? Au una define vp karma? watu wanasubiri Makonda nae akamatwe,
Nadhani kila mtu ana uhuru wa kucomment. Usiwalazimishe watu kuwa na mahaba yasiyo na macho. Mama anafanya vizuri lakini kama watangulizi wake sio malaika
 
Karma ilimshughulikia Magufuli,kifo si adhabu, lakini ukifa kabla ya muda wako inakuwa adhabu....Azory Gwanda na Ben Saanane waliuawa kwa baraka za Magufuli

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
[emoji115]BS
 
I am confused. Sielewi Pascal anataka nini. Tuache kuwalaani wale tuliombiwa dhahiri shahairi kuwa walitenda uhalifu chini ya mwendazake kwa msingi kwamba wapo ambao hatujawajua. Sisi tutashughulika na wahalifu kadri tunapopata tuhuma/ushahidi na kujiaminisha kuwa kuna dhuluma ama uonevu umefanyika.
 
Hakika umeandika ukweli mtupu. Kama ni kushughulikia ya awamu iliyopita yashughulikiwe yote na si kubagua kwa maana yalitokea chino ya usimamizi wa utawala ule ule
 
Chonde chonde, hata hili la Wamachinga, jinsi tunavyowafanya sasa, JPM anawaona. Musukuma na Polepole wako right. Wamachinga watendewe haki.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…