Life span ya tyre ni miaka mingapi?

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Naomba kuuliza maswali haya kwa wenye uzoefu wa magari.
1.Tyre ukiichukua mpya ukaifunga ukaitembelea au hata upaki gari yako uani inatakiwa idumu miaka mingapi ndio ubadili?Hata kama kashata zipo
2.Kuna aina nyingi za matairi mfano Yokohama,Michelin,Firestone,Bridgrstone,General tyre,Trentyre na mengine mnayojua je ni yapi bora zaidi?
Nawasilisha kwa faida yangu na wote wajuzi ingieni hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kawaida "LIFE SPAN" ya tairi inahesabiwa kwa KILOMETA (KM) mkuu, si kwa miaka. Na tairi inategema na "QUALITY" ya watengenezaji, kuna watengenezaji wa tairi za quality ndogo na quality za juu (ndio maana hata bei huwa zinatofautiana kutokana na quality).

Huo ndio ufahamu wangu mkuu.
 
Ahsante ngoja wengine waje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lifespan ni miaka 4! Na inaweza ika expire hata kama hujaitumia.... ukitaka kununua angalia tyre utakuta limeandikwa mwaka wa kutengenezwa. Ikifika miaka 4 inakua ndio mwisho wa matumizi hata kama hujaitumia (ina expire)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo sahihi mkuu. Ubora wa tairi haupimwi kwa kilometers. Tairi nyingi Miaka haitakiwi kuzidi minne tangu siku ya kutengenezwa ila nadhani Kuna baadhi zinasogea mbele kidogo.
Tairi inaweza ikawa dukani ukaiona ni Mpya kumbe tayari imeisha mida wake wa matumizi. Tairi zote huandikwa mwezi na mwaka lililotengenezwa. Ukikagua tairi utakuta limeandikwa tarakimu nne mfano 0912 hapo utajua limetengenezwa wiki ya tisa Mwaka 2012. Ko ukijumlisha Miaka minne mbele mwisho wake ni 2016. Na unaweza ukalikuta dukani jipya Mwaka huu 2020 ukaingia chaka.
 
TBS wanadai kwamba umri wa matairi ni miaka 8. Cheki standard numbers: TZS 617:2009 na TZS 618:2009 kwa pneumatic tires for trucks/buses na passenger cars respectively.
 
Kuna tyre huwa hazina noma kama BF life span yake ni miaka 6 ila huwa inasogea mpaka miaka 8 bila kuleta mushkeli yoyote
 
Upo sahihi sana, ingawa ninavyofahamu life span ya tairi ni miaka mitano badala ya minne
 
Sio kweli. Tairi huwa inapimwa ubora wake kulingana na muda imekaa tokea kutengenezwa. Nadhani ni miaka mitano kama sio minne.

Tairi ikikaa muda huo hata kama haikutumika inakuwa haifai tena. Ndio maana kuna muda unaenda dukani kununua tairi mpya ila ukianza itumia pancha kila wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…