Lift nayompaga Workmate imezua utata!!!

Mweleweshe gf wako kuwa ni lift 2 na hamna mengineyo asipokuelewa acha kutoa lift hiyo
 

Kaa chini na mkeo mweleze vizuri ikiwezekana mkutanishe na huyo dada,kama ataelewa endelea kumpa lifti huyo dada asipokuelewa acha kumpa lifti na pia kama mkeo ameshakugundua wewe ni choma choma na ushakuwa na mahusiano nje ya ndoa awali,hawezi kukuamini pengine wewe ni kama Simba akiona swala tu kosa! Sasa mkeo anahofia lifti inaweza kuwa lifti kweli!
 

yan we acha neylu, hiko ndo kilichontokea mie. nikanyimwa lifti hivi hivi. duh inabidi ninunue hata kibajaj lol. . . .
 
Last edited by a moderator:
yan we acha neylu, hiko ndo kilichontokea mie. nikanyimwa lifti hivi hivi. duh inabidi ninunue hata kibajaj lol. . . .

My dear, na kweli nunua hata kibajaji maana wivu wa mke akijilinganisha hafanani na wewe hata kwa kuigiza, akaona dawa ni kukubania usipande lift ya mumewe....... Angejua huko kazini mwaonana kila dakika, na mkiamua kufanya lolote mnafanya.. Maaaskini yao wanaokosa kujiamini.. Lol
 
Inategemea kama uko smart kiasi gani katika mapenzi juu ya huyo girlfriend wako, ila kama ndiyo unatoka na huyo dada wa ofsn ni balaa jingine. Ni ukweli wako pekee ndiyo usalama wa mapenzi yenu otherwise ni kazi bure... Pole mkuu.
 
Anao kwa mbali sana, mpaka aone nimempa lift kwa miaka 3 hivi ndo wivu unamwingia.......

Maana tajiuliza miaka mi 3 yote hajapata hata kabajaj cha kummuvuzisha job?.....

daaah huyo safi sana...... wengine mpaka anastaafu hata baiskel hakuna kwa hiyo unapiga tu
 
Huyo rafiki yako naye ana roho mbaya kweli! Au pengine labda ni kutojiamini tu! Sasa watu ni majirani na mnafanya kazi sehemu mmoja, unaanzaje kumnyima lift kisa jinsia yake tu?

Ahsante sana, angalau uko upande wangu!!

Mimi nakaa Sinza Vatican, nae anakaa Sinza white-inn.
Ofisini ni Kurasini ambapo kwa daladala inabidi upande daladala mbili kama wapitia Kariakoo, au tatu kupitia posta.

Tena kwa njia ya kariakoo ukishuka kituo cha kwanza kuna umbali mrefu mpaka mabasi ya kituo cha pili yanapoanzia.

Mimi kumpa lift hainiongezei gharama za mfuta, sanasana inanipunguzia upweke garini.

Sasa wifi/shemeji yenu anadai kama nampenda huyo workmate niseme
 
Reactions: SMU
Effort is important,
but knowing where
to make an effort
in your life
makes all the difference

tafakari.............
 


Dah.........unahuruma sasa wewe..................haya chagua moja!
 
Kaa naye, mwambie ajifanye ni huyo workmate wako aangalie anavyopata shida ya kuunganisha daladala halafu mwambie kama ungekuwa chomachoma usingemweleza ingawa nadhani ulichelewa kumwambia mapema. Akumbuke wimbo wa h. Kalala wa lift.
 
Kwani ukiwakutanisha kuna nini?


huyo anaepewa lift anakutega?

My Girlfriend Sikai nae, but juzi kati alikuja akambonji kwangu, then asubuhi akaona call from workmate ikinitaarifu kua ashafika kituoni.

Ye hataki kukutana nae, bali nsitoe lift au tuachane!!
 
Huruma itakuponza baba. Ndio ni vizuri kumpa mtu wa jinsia tofauti lakini inabidi uwe na kiasi sio kila siku yeye tu na wewe kwenye gari kuelekea ofisini. Gf wako yuko sahihi kabisa, ungekuwa unampa huyo dada lifti mkia na Gf wako kwenye gari isinpekuwa shida. Katika mapenzi usiruhusu mazingira ya kumfanya mpenzi wako akuhisi vibaya ita kucost. Au jifanye wewe ndo unaona yeye kila siku anampakia workmate wake mwanaume.
 
kama ni lazima sana kumsaidia mlipie nauli mkuu,otherwise yeye ni wakupita tu...unless upo na interest naye kaka...

Mkuu,
Usafiri wa Dsm asubuhi na Jioni tatizo lake sio nauli.
Nauli unayo na Basi hupandi.
Ofisini kuna mambo mengi, naweza kupata dharura nikmtumia yeye kama back-up yangu.

Sasa najiskia vibaya sana kumfanyia Roho Mbaya sababu tu za hisia za Gf wangu.
 
khee.. kwa hiyo adi number ya simu mmepeana mnaambiana kua kafika kituoni? basi gfriend wako hana makosa bora asingekupigia simu who knows mtakua mnaambiana tu kuhusu kufika kituon, safari moja huanzisha nyingine
 
My Girlfriend Sikai nae, but juzi kati alikuja akambonji kwangu, then asubuhi akaona call from workmate ikinitaarifu kua ashafika kituoni.

Ye hataki kukutana nae, bali nsitoe lift au tuachane!!

wakutanishe.watambulishe
 
Mi wala simshangai girl friend wako. Mtu chake bwana.

Yani umefikia kupigiwa na simu ...wewe umekuwa dereva wa huyo binti???

Mimi mume wangu analijua hilo...marufuku kuwapa mabinti lifti...labda..tena labda wamama watu wazima jirani ninao wafahamu...nayo siyo ndo iwe kila siku.

Hata yeye hatanivumilia nikiwa nampa lifti jamaa fulani kila siku.

Lift lifti mwisho LIFT


My Girlfriend Sikai nae, but juzi kati alikuja akambonji kwangu, then asubuhi akaona call from workmate ikinitaarifu kua ashafika kituoni.

Ye hataki kukutana nae, bali nsitoe lift au tuachane!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…