Ligi Daraja la Kwanza 2014/15, updates hapa

Mlendamboga

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
667
Reaction score
338



Ligi Daraja la kwanza ni ngazi ya pili Kitaifa katika mashindano ya mpira wa miguu nchini Tanzania. Hukutanisha pamoja timu 18 kutoka sehemu mbalimbali nchini kwa minajili ya kutoa timu tatu ambazo zitapanda daraja kwenda Ligi Kuu ya Vodacom. Timu zinazoshuka kutoka Ligi Daraja la Kwanza huenda Ligi ya Taifa, ambapo timu tatu hupanda kila msimu kuja Draja la Kwanza.

Timu tatu zilizopanda daraja kwenda Ligi Kuu msimu huu ni

1.Ndanda FC
2.Polisi Morogoro
3.Stendi United


Msimamo wa makundi hadi leo tarehe 17 Februari 2015

Kundi A **Klabu za African Sports na Majimaji zimepanda daraja rasmi baada ya kushika nafasi mbili za juu katika Kundi A

KUNDI B **Klabu za Mwadui na Toto Afrika zimepanda daraja baada ya kushika nafasi mbili za juu kwenye kundi B

© Tovuti Rasmi ya Shirikisho la Soka Tanzania
 
Saaafi, nami nitakuleteeni kutoka mpakani na Zambia ambako villa squard wanakuwa wageni wa kimondo ssc
 
Kimondo wanapata bao la kwanza dakika y 41 kupitia kwa Geofrey Mlawa ambaye ni captain wa timu hiyo baada ya makosaya beki wa. villa Squard.

Nurdin Bakari ambaye ni captain wa timu anaonekana uzee unamkabili akili inataka mwili umegoma. Kwaujumla Villa kiwango chao ninkizuri wanakuja vyema ingawa kimondo wamekuwa na mchezo wa spidi na kutumia wingi zaidi hali inayowachosha villa.

Uzi mpya wa rangi maalumu kama ilivyokuja mbeya city ndivyo kimondo wameanza ligi kwa kutambulisha jezi za blue bahari ambayo mashabiki wameonyesha kuipenda. villa wamevaa rangi za Simba Nyekundu zenye ufito kwenye bukta wa njano

Mpira ni mapumziko
 
Kimondo inspata bao la 2 kwa njia ya pernati kupitia kwa Mpoki baada ya mchezaji wa kimondo kuvutwa mikono akiwa anaenda kumsalimia kipa wa villa
 
Villa dk 89 walikosa penati baada mchezaji kuangushwa eneo la hatari lakini maajabu mtu akapiga nje penati
 
Hadi mwisho Kimondo 2 Villa squard 0 uwanja wa Ccm vwawa
 
La ajabu tiketi zilizotumika ni za mechi ya simba vs zimamoto
 
hongera toto wanakishamapanda wa mwanza....kaza buti tunakuhitaji sana ligi kuu
 
15/10/2014 kundi a"

kimondo ssc 2 vs ashanti united 0 uwanja wa ccm vwawa
kurugenzi fc vs polisi dar uwanja wa mufindi
african sports 0vs lipuli fc 0-uwanja wa mkwakwani
friends rangers fc 1 vs african lyon fc 0 uwanja wa karume dsm
jkt mlale 1 vs villa squard 0 uwanja wa majimaji -ruvuma


kama kawaida wanamichezo walioko viwanja mbalimbali hapa endelea kutupia maendeleo ya michezo hiyo

kundi b

geita 0 vs rhino rangers 1 uwanja wa nyakumbu sec
toto african 2 vs burkina faso 1- uwanja ccm kirumba
jkt oljoro 0 vs jkt kanembwa 1 - uwanja wa sheikh amri abeid arusha
panone 1 vs mwadui 1 fs uwanja wa ushirika kilimanjaro
polisi mara 1 vs green worriors 0 uwanja wa karume dar
polisi tabora 0 vs polisi dodoma 1uwanja wa ali hasan mwinyi
 
15/10/2014 kundi a"

Kimondo ssc vs Ashanti united uwanja wa ccm vwawa
Kurugenzi fv vs Polisi dar uwanja wa mufindi
African sports vs Lipuli fc -uwanja wa mkwakwani
Friends rangers fc vs African lyon fc uwanja wa Kkarume dsm
Jkt mlale vs Villa squard uwanja wa majimaji -Ruvuma

kama kawaida wanamichezo walioko viwanja mbalimbali hapa endelea kutupia maendeleo ya michezo hiyo

kundi b

geita vs rhino rangers uwanja wa nyakumbu sec
toto african vs burkina faso- uwanja ccm kirumba
jkt oljoro vs jkt kanembwa - uwanja wa sheikh amri abeid arusha
panone vs mwadui fs uwanja wa ushirika kilimanjaro
polisi mara vs green worriors uwanja wa karume dar
polisi tabora vs polisi dodoma uwanja wa ali hasan mwinyi

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…