Ligi Daraja la Kwanza 2014/15, updates hapa

Uwanja wa ccm vwawa ni mapumziko Kimondo 0 Ashanti 0
 
Kimondo anaongoza kwa bao 1 mpaka sasa Ashanti bado biashara ngumu ingawa kiwango chao si cha kupuuza
 
[h=3]ASHANTI MAJANGA" YAAMBULIA KICHAPO CHA 2 KAVU KUTOKA KIMONDO [/h]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Kikosi cha ASHANTI kilichoshuka dimbani dhidi ya Kimondo na kuambulia kichapo cha 2 Oclock[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Hii ndiyo sumu ya Ashanti al maarufu kama Kimondo KISSC iliyoshuka jioni ya leo na kutoka na ushindi wa mabao matakatifu 2-0[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Benchi la Kimondo


Na Indaba Africa,



Ikicheza uwanja wake wa nyumbani Kimondo SSC ya Mbozi imeendelea kutunisha msuri kwa timu za maji ya chumvi , mara hii kwa kuibatua Ashanti United mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliofanyika uwanja wa CCM Vwawa.
Hadi mapumziko , si Kimondo wala Ashanti walikuwa wamechungulia nyavu za timu pinzani licha ya Kimondo kukosa mabao matatu ya wazi katika gonga zilizochezwa kwenye lango la ASHANTI lakini papara za wachezaji wake ziliiharibu mabao hayo.
Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko ya mfulizo yaliyofanywa na kocha wa timu ya Ashanti ambayo yaliongeza uhai na mashambuzi, gonga na viminyo vya hapa na pale, hata hivyo michezo ya kimjini mjini –zikiwemo rafu za hapa na pale, vipepsi na janja janja ziliwagharimu Ashanti kwa wachezaji wake wawili kupewa kadi za njano kwa kuwajeruhi wachezaji wa kimondo ambao mmoja alishindwa kuendelea na mchezo.
Mnamo dakika ya 72 Kimondo kupitia kwa Michael Mwailusu Bosco baada ya kutokea gonga nikugonge langoni mwa ASHANTI kufuatia kona iliyopigwa na Mshaki Simbeye
Dakika ya 89 Kimondo walitupia msumari wa moto langoni mwa Ashanti ulioenda moja kwa moja wavuni bila mlindamlango kuuona mpira ulioanzia wingi ya kushoto , bao lililofungwa na Geofrey Mwashuya ambaye katika mchezo huo alionekana wazi kuwa hatakuwa na timu ya Kimondo kwenye dirisha dogo la usajiri kutokana na kiwango chake kuendelea kuvutia timu nyingi za ligi kuu.
Ama kwa upande wa mashabiki, burudani ya mchezo wa leo iliongezewa chachandu baada ya mashabiki wa Mbeya City kukodi mabasi mawili kuja kuipa sapoti Kimondo ya Mbozi hali ambayo iliufanya uwanja ulindime kwa shamra shamra na mbwebwe za mashabiki hao.
Mchezo wa leo uliochezeshwa na mwamuzi Kinugani kutoka Morogoro akisaidiwa na Alphaxad Mteta kutoka Ruvuma, Cheyo kutoka songea , Kefa kayombo kutoka mbeya ulikuwa chini ya kamisaa Zahra Mohamed mwamuzi wa siku nyingi wa michezo ya kimataifa.
 
Leo jumapili kundi B kuna mechi kati ya Kimondo Vs Kinondoni Municipal Council KMc ambao wamebadili jina la awali la TESSEMA. Mchezo utafanyika uwanja wa Ccm Vwawa.Kimondo mpaka sasa imeshinda michezo yake miwili kwa ushindi unaofanana wa bao 2-0 kila mchezo hivyo kuwa na pointi 6 mabao 4 huku ikiwa haijaruhusu bao kwenye nyavu zake! Wakati Tessema hali yake taabani kwa kufungwa michezo yake miwili
Iliyocheza
 
yani ktk ligi hii ukiwa home usiposhinda basi tena.

Malalamiko yake yalikuwa na msingi, lakini sidhani kama alivyoawakilisha ni sawa. Yani ni kama TFF na Bodi ya Ligi wameunda mkakati maalumu kwa ajili ya timu yake tu, hisi zilikuwa nyingikuliko uhalisia.
 
Malalamiko yake yalikuwa na msingi, lakini sidhani kama alivyoawakilisha ni sawa. Yani ni kama TFF na Bodi ya Ligi wameunda mkakati maalumu kwa ajili ya timu yake tu, hisi zilikuwa nyingikuliko uhalisia.

inawezekana madai yake yanaukweli maana jamaa ana bifu na tff na bodi ya ligi tokea wamzingue kutumia jezi za zantel.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…