Ligi Daraja la Kwanza kuchezwa makundi matatu 2015/2016

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2015/2016 itachezwa katika makundi matatu ya timu nane nane kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Mfumo huo wa makundi matatu umetokana na marekebisho ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) yaliyofanywa hivi karibuni na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao cake kilichofanyika mjini Zanzibar.

Timu ya kwanza katika kila kundi la ligi hiyo itakayoanza Septemba 12 mwaka huu itapanda kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa msimu wa 2016/2017 wakati timu itakayoshika nafasi ya mwisho katika kila kundi itashuka kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa msimu wa 2016/2017.

Kundi A linaundwa na timu za African Lyon FC (Dar es Salaam), Ashanti United SC (Dar es Salaam), Friends Rangers FC (Dar es Salaam), Kiluvya United FC (Pwani), Kinondoni Municipal Council FC (Dar es Salaam), Mji Mkuu FC (Dodoma), Polisi Dar es Salaam na Polisi Dodoma.

Timu zinazounda kundi B ni Burkina Faso FC (Morogoro), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mafinga FC (Iringa), Lipuli FC (Iringa), Njombe Mji FC (Njombe), Polisi Morogoro na Ruvu Shooting (Pwani).

Kundi C ni Geita Gold SC (Geita), JKT Kanembwa FC (Kigoma), JKT Oljoro (Arusha), Mbao FC (Mwanza), Panone FC (Kilimanjaro), Polisi Mara, Polisi Tabora na Rhino Rangers (Tabora).

Imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
 
kuna timu shiriki nyingi sana huma kama hao bukina faso.
 
Huku ni kupanga Matokeo Haiwezekani timu za Da es salam zote ziwe kundi moja Wadau..
 
Huku ni kupanga Matokeo Haiwezekani timu za Da es salam zote ziwe kundi moja Wadau..

Ni bora hivyo maana wanaweza kuwekwa makundi tofauti kisha wrote wakaongoza makundi zitapanda zote za dar..... Huoni hapo imetoa ahueni kwa timu za mikoani!!???
 
Ni bora hivyo maana wanaweza kuwekwa makundi tofauti kisha wrote wakaongoza makundi zitapanda zote za dar..... Huoni hapo imetoa ahueni kwa timu za mikoani!!???

Msimu uliopita hakuna timu ya Dar hata moja iliyopanda daraja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…