Ligi daraja la kwanza ni ngumu kuliko ligi kuu, TPL

Ligi daraja la kwanza ni ngumu kuliko ligi kuu, TPL

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Posts
5,039
Reaction score
6,253
Yes...
Kabla ya kufika ligi kuu TPL kwa mpira wa hapa kwetu Tz lazima upitie ngazi za chini, yaan uanze ligi daraja 4,3, 2(ngazi mkoa) na 1, huko kote timu inaweza kupambana hadi kufika ligi daraja la kwanza....
Ugumu huja pale ambapo timu inataka kupanda ligi kuu, figisu figisu hua zinakua nyingi sana, baadhi ya wanasiasa hutumia mpira kama ngazi ya kupanda kisiasa...
Kuna wanasiasa hutoa ahadi kipindi cha kampeni kwamba nikishinda nafasi fulani basi nitahakikisha tunapata timu ligi kuu....
Hivyo hutumia nguvu na madaraka kuhakikisha timu inapnada katika mikoa au majimbo yao ,
Soka ni mchezo wa wazi, Lakini unaweza kupangiwa mwamuzi ambaye hafuati misingi ya soka na hafuati sheria 17 za soka,
Jana nilibahatika kumsikiliza Hery Mzozo mmiliki wa timu ya Friends Rangers ya pale Magomeni alipokua akihojiwa na Efm radio, Mzozo alilalama sana kiasi cha kusema timu yake ilistahili kupanda ligi siku nyingi lakini waamuzi wanawaangusha, kingine wapo viongozi wa mpira hawataki kuisaidia timu hiyo ,
Mfano friends Rangers walikua na mechi na Namungo FC ya pale Ruangwa Lindi, Mzozo anasema walikua ni watu 23 tuu ndio walienda Lindi na hakuna kiongoZi hata mmoja wa mkoa wa Dar es salaam ambaye aliambatana na timu....

Nasisitiza ligi daraja la kwanza ni ngumu tena ni ngumu sana, bila kumuona mwamuzi ligi kuu utaisikia tuu, nakumbuka kipindi nipo chuo tulishiriki SHIMIVUTA mashindano ya Taasisi ya elimu ya juu, pale mkwakwani mpira ulikua unachezwa katikati ya u2anja mda wote, refa hakupewa mlungula hivyo alikua anatuadhibu....

Nitoe wito kwa wadau , Soka ni mchezo ambao unapendwa sana duniani , hivyo haki itendeke hususani kwenye maamuzi ili tupate washiriki wa kweli na kutengeneza timu ya taifa ambayo itafanya vizuri kimataifa,
 
Back
Top Bottom