Ligi Kuu Bara | Mbeya Kwanza FC Vs Simba SC | Uwanja wa Majimaji | Juni 29, 2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Wanajulikana kuwa ni watalaamu wa kusakata Kabumbu Nchini Tanzania lililothibitishwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF, Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, leo Juni 29, 2022 yupo ugenini kwenye Dimba la Majimaji kupambana na Mbeya Kwanza FC katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo leo inafikia kikomo kwa Timu zote kujitupa kwenye viwanja tofauti kucheza michezo ya mwisho.

Matokeo ya leo kati ya Mbeya Kwanza FC dhidi ya Simba SC hayawezi kuathiri kwa vyovyote msimamo wa Ligi Kuu, ambapo Mbeya Kwanza FC tayari ameshashuka daraja rasmi huku Simba SC akijihakikishia nafasi ya pili

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10:00 Jioni.. Usikose Ukaambiwa

Kulipewa Mwana...Kulitaka Mwana



======

05' Mpira umeanza Uwanja wa Majimaji kwa kila timu kucheza mpira nzuri.

10' Hakuna timu imeona lango la wenzake, huku Simba wakimiliki mpira, lakini Mbeya Kwanza wanatibua mipango yote ya Simba SC

15' Kennedy anamrudishia golikipa Beno, lakini anaukosa na mpira unaambaa ambaa unatoka nje, ilikuwa nafasi nzuri kwa Mbeya Kwanza kufunga

Free Kick kuelekea Mbeya Kwanza FC, inapigwa kulee lakini mpira unaokolewa na mabeki wa Kwanza FC

20' Beno anafanya balaa anaokoa hatari ambayo almanusura Mbeya Kwanza wapate bao, mpira imetoka nje na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

25' Kassim anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali kuelekea Mbeya City, mpira wake umepaa juu ya lango.

30' Jaribio la maana sana, kwa Mbeya Kwanza lakini mpira wa Mpepo unagonga mwamba wa juu na kurudi Uwanjani.

Simba wanajibu Counter mbele kuleee lakini Kibu anakosa nafasi nzuri ya kufunga kwa mpira kuokolewa, ilikuwa nafasi murua hii.

35' Mhilu anapiga pasi hafifu kwa mlengwa, ambayo inakuwa kama chakula kwa mabeki wa Kwanza FC kuokoa.

42' Simba wanashindwa kutumia nafasi nzuri ya kufunga kwa mpira uliopigwa na Kibu kuambaa ambaa eneo la hatari na kuokolewa na beki wa Kwanza FC.

45+1' Kuelekea kuwa mapumziko ambapo hakuna timu imeona lango la wenzake.

Naaam mpira ni mapumziko | Mbeya Kwanza FC 0-0 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Majimaji, huku mapema tu Simba wakikosa kutumia nafasi ya kufunga huku wakipata Kona mbili ambazo hazikuzaa bao.

53' Nyoni anapiga free kick kuelekea Kwanza FC, lakini golikipa anatokea na kudaka bila wasiwasi.

59' Jimmy anakosa nafasi nzuri ya kufunga, baada kupiga shuti dhaifu na mpira kuokolewa.

Almanusura Kwanza FC waandike bao, kama angekuwa makini mchezaji Richard angefunga

65' Simba wanapata Free Kick eneo nzuri na wanashindwa kutumia nafasi hiyo.

66' Kwanza FC wanakosa nafasi tena baada ya mchezaji kuwa 50+50 na golikipa Beno, lakini mpira unaokolewa na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

75' Timu zote zinacheza kwa kushambulia kwa zamu huku mabeki wakiwa imara kwa pande zote mbili

Kibu yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kupata rabsha, ameinuka mpira unaendelea

83' Ametoka Mhilu na nafasi yake imechukuliwa na Bocco.

88' Kwanza FC wanashindwa kutumia nafasi ya kufunga, ilikuwa Shambulizi kali kuelekea lango Simba

90+2' Kuelekea kumalizika kwa mchezo, milango bado ni migumu hakuna mbabe.

Free Kick anapiga Chuku, Ooooh mpira unaokolewa na Gadiel, ilikuwa nafasi murua kujipatia bao dakika hizi za mwisho.

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Timu zote zimetoka sare, zimegawana alama.

FT: Mbeya Kwanza FC 0-0 Simba SC

...... Ghazwat...
 
Leo Kibu anapiga hat trick yake ya kwanza
 
15' Mchezo unaendelea huku kila timu kucheza mpira nzuri, lakini hakuna ambaye ameona lango

Mbeya Kwanza FC 0-0 Simba SC
 
Umesoma heading vizuri lakini?
Leo ni siku ya mwisho ya kufunga hesabu! Hakukuwa na sababu ya kuleta uzi wa simba pekee. Mtoa mada angeleta uzi wa matokeo ya timu zote, ingependeza sana.
 
Umesoma heading vizuri lakini?
Sijasoma heading ila nimesoma fixture ya leo nikaona kuna mech ya Mayele na Mtibwa.

Hii mechi ya Mbeya mwisho na Simba haina mvuto. Inajulikana Simba itashinda kigoli kimoja cha offside au Mbeya Mwisho watajifunga
 
Hadi kufikia mapumziko matokeo ni haya kwa Timu zote za Ligi Kuu
 
Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Majimaji | Mbeya Kwanza FC 0-0 Simba SC
 
Leo ni siku ya mwisho ya kufunga hesabu! Hakukuwa na sababu ya kuleta uzi wa simba pekee. Mtoa mada angeleta uzi wa matokeo ya timu zote, ingependeza sana.
Kwenye Uzi kuna sehemu..Ligi Kuu inafikia kikomo kwa Timu zote kucheza michezo ya mwisho.

Weka Updates kwa matokeo mengine hapa.
 
Ametoka Mhilu na ameingia Bocco upande wa Simba SC

83' Mbeya Kwanza FC 0-0 Simba SC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…