Ligi Kuu Bara: Yanga vs Simba - Uwanja wa Taifa (1-1)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426

Mpaka muda huu uwanja unaelekea kunona , mashabiki wa pande zote mbili wanazidi kumiminika .

Mashabiki maandazi nao wamo pia , kama kawaida rangi nyekundu na zile za njano zimetawala mitaa .

Tuwe pamoja kwa live coverage hapa hapa jukwaani.

Nakala imfikie OKWI BOBAN SUNZU .
..........................................................
Matokeo: Simba 1 - Yanga 1
90' Simba 1 - Yanga 1


Goal: Kichuya
87' Simba 1 - Yanga 1
83' Simba 0 - Yanga 1
Yanga Sub | Juma Mahadhi OUT Simon Msuva IN
Yanga Sub | Deus Kaseke OUT Haruna Niyonzima IN
Simba Sub | ibrahim Ajib OUT Ibrahim Mohammed IN
72' Simba 0 - Yanga 1
Simba Sub | Laudit Mavugo Out Blagnon IN
Simba Sub | Lufunga OUT Juuko Murshid IN
60' Simba 0 - Yanga 1
Kipindi cha pili kimeanza
45' Mpira umerejea kutoka mapumziko, Yanga anaongoza kwa goli moja
45+9' Mpira unaenda mapumziko
29' Jonas Mkude anapokea kadi Nyekundu
28' Mashabiki wengi wa Simba wanakimbia kutoka uwanjani baada ya upande wao kurindima mabomu ya machozi.
28' Mabomu ya machozi yanapigwa baada ya mashabiki kuanza kuvunja viti na polisi kujibu mapigo.
27' Kuna sintofahamu baada wachezaji wa Simba kumvaa Mwamuzi



26' Goooal, Yanga anatangulia kwa kufunga goli la kwanza kupitia kwa Amis Tabwe
00' Refa anapiga filimbi kuashiria mwanzo wa mchezo
Mengineyo - Kutokana na utaratibu mpya wa kupata tiketi basi bila shaka tutarajie kuvunjwa kwa rekodi ya mapato , sitarajii visingizio vya namna yoyote ile .
..............................................
Tathmini yangu baada ya ya Dk 70 , Yanga ya leo isingeiweza Simba kama wachezaji wote 22 wangekuwa uwanjani .

Dk 90 zimemalizika , Yanga 1 - 1 Simba ,

Asanteni kwa kutufuatilia .
 
Chanel gani inaonesha ? Naona Azam 2 washakua offline wakat asubui walikua wanapatikana fresh...
 
nimeona line up ya timu zote mbili, yanga anashinda ila kama atafungwa au kudroo naomba lawama zote zimwendee Hans Van da Plujim kwa kupanga kikosi kama alivyopanga, kwa kumweka benchi dida, dante, na niyonzima. dante hayupo kabisa ata benchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…