Ligi Kuu Kenya yahitimishwa, Gor Mahia wamepewa ubingwa

Mambo ya ubingwa wa mezani yalisha pitwa na wakati. Timu ya mwisho kupewa ubingwa wa mezani walikua Mtibwa baada ya waziri wa michezo Kapuya kutumia ushabiki wake wa Simba kuwapora Ubingwa Yanga na kuwapa Mtibwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wao kanuni za ligi zinasema

"Endapo ligi itasimama na itashindwa kuendelea kwa sababu yoyote ile, na timu zote zikiwa zimeshacheza mechi zote za mzunguko wa kwanza, timu inayoongoza ligi itatangazwa bingwa"

Kanuni za ligi ya VPL zinasemaje kuhusu ligi yetu kutoendelea [emoji23][emoji24][emoji23][emoji24][emoji23]

Acheni kupenda vya mteremko nyie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mteremko gani? Wa kanuni sio, maana kama ni uwanjani simba tayari ni bingwa. Halafu hizo kanuni wewe mwenyewe huzijui sasa kwa nini unasema mnyama anapenda mteremko?
 
Simba bingwa wa nini? Points zake haiwezi kufikiwa na timu yoyote kwa sasa?

Sibahatishi na nina uhakika kwamba kanuni za VPL zimekaa kimya kuhusu nani awe bingwa kwa mazingira kama haya yaliyojitokeza ya ligi kutoendelea

Kwenye ligi ya Kenya kanuni zinatoa mwanya wa Gormahia kutangaza bingwa

Acheni kupenda mteremko nyie
Mteremko gani? Wa kanuni sio, maana kama ni uwanjani simba tayari ni bingwa. Halafu hizo kanuni wewe mwenyewe huzijui sasa kwa nini unasema mnyama anapenda mteremko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timu zote zipewe point 3 magoli matatu kwenye mechi zote zilizo baki.
Mwenye point nyingi atangazwe bingwa.
 
Mapendekezo yako ni yapi? ila kumbuka yule ambaye matumaini yake ni FA ili awakilishe kimataifa ligi ikifutwa atakuwa amepata mteremko.
 
Mteremko gani? Wa kanuni sio, maana kama ni uwanjani simba tayari ni bingwa. Halafu hizo kanuni wewe mwenyewe huzijui sasa kwa nini unasema mnyama anapenda mteremko?
Wacha kupenda kitonga mkuu itakuponza, toka jasho hadi mwisho upate vya halali
 
Mapendekezo yangu ni

Ligi imaliziwe

Mazingira yakiwa sio rafiki

Ligi ifutwe

Maana kwa mujibu wa Kanuni bingwa anapatikana baada kila timu kucheza na kila timu nyumbani na ugenini na anayemaliza mechi zote akiwa na alama nyingi zaidi ndio anakuwa bingwa
Mapendekezo yako ni yapi? ila kumbuka yule ambaye matumaini yake ni FA ili awakilishe kimataifa ligi ikifutwa atakuwa amepata mteremko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kwa mapendekezo yako ila kama kuna kanuni za kumtangaza bingwa kwa mazingira kama haya huo sio mteremko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…