Ligi Kuu soka nchini Ufaransa yafutwa kutokana na CoronaVirus. Maamuzi ya PSG kupewa Ubingwa au la kujulikana Mei

Ligi Kuu soka nchini Ufaransa yafutwa kutokana na CoronaVirus. Maamuzi ya PSG kupewa Ubingwa au la kujulikana Mei

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Ligi Kuu Soka nchini Ufaransa (The Ligue 1) na Ligi Daraja la Pili (Ligue 2) zimefutwa baada ya Waziri Mkuu wa nchini hiyo kusema michezo yote itatakiwa kuendela Septemba 2020

Amesema kuwa michezo yote iwe inachezwa bila mashabiki au na mashabiki haitaweza kuendela nchini humo kabla ya Septemba mwaka huu

Ligue 1 na Ligue 2 zilipanga kuendelea kuchezwa Juni 17, 2020 huku Shirikisho la Soka Ulaya likiweka hadi Agosti 2, 2020 kuwa Ligi zote za ndani barani humo ziwe zimemalizika

Shirikisho linalozimamia Ligi hizo limepanga kukutana Mei 2020 ili kujadili ni kwa namna gani msimamo wa ligi utatafsriwa na timu zipi zitashuka daraja na zipi zitapanda daraja

Pia, watajadili timu gani zitapata nafasi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya na kama PSG inayoongoza Ligi hiyo kwa alama 12 hadi sasa itawazwe kuwa Bingwa
 
Epl may 4 mazoezi yanaanza ,may 15 ligi inarudi bila mashabiki
Tunasubiri hukumu ya epl

Tunawe mikono kwa wingi

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Back
Top Bottom