Tuwe pamoja kwa updates za mechi ya Azam na Yanga itakayochezwa uwanja wa Chamazi Complex
Kikosi cha Azam
Razack Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Agrey Moris, Yakubu Mohamed, Stephan Kingue, Joseph Kimwaga, Salum Abubakar, Bernard Arthur, Shabani Chilunda, Enock Atta.
SUB: Mwadini, Mwantika, Kheri, Hoza, Kipagwile, Mbaraka, Paul Peter
Kikosi cha Yanga
Youthe Rostand, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Andrew Vicent, Kelvin Yondani, Said Juma, Raphael Daud, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib, Emmanuel Martin.
SUB: Kabwili, Mwinyi, Maka, Mahadhi, Mussa, Matheo, Mwashiuya.
1' Kipyenga kimelia kuashiria gemu imeanza
2' Mpira umeanza kwa presha timu zote zikishambuliana kwa zamu
4' Gooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Azam wanapata bao la kuongoza baada ya mabeki wa Yanga kufanya makosa na Shabani Chilunda kutumia nafasi hiyo kupachika bao la kuongoza.
7' Yanga wanafanya shambulizi la kushtukiza kupitia kwa kiungo wake Papy Kabamba Shishimbi lakini Kipa anainyaka kabla haijaleta madhara
10' Shaban Idd Chilunda anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kucheza rafu
15' Yanga wanafanya shambulizi baada ya Shishimbi kupiga shuti matata hadi likamshinda goli kipa, lakini akaliokoa
16' Yanga wanapigia huku wakishambulia lango la azam lakini Ajib anaharibu mahesabu hapa.
21' Salum Abubakar anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumcheza madhambi, faul inapigwa kuelekea lango la azam.
28' Ibrahim ajibu anapiga shuti kali katika lango la azam, lakini kipa anadaka kwa ustadi
30' Goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Obrei Chirwa anapachika goli la kwanza baada ya kupokea pasi toka kwa Ibrahim Ajibu ambapo alimbabatiza kipa na kufanikiwa kuondoka na mpira na kupachika goli la kusawazisha.
35' Emmanuel Martin anafanya shambulizi kwenye goli la Azam, lakini inakuwa ni goal kiki.
36' Azam wanamtoa Bernad Arthur anaingia Hoza
38' Azam wanapata kona ya kwanza
39' Shaban Idd Chilunda yupo chini na sasa anapatiwa huduma ya kwanza.
40' Faul inapigwa kuelekea lango la azam
43' Steven Kingwe anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kucheza
44' Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Gadiel Michael Mmbaga anapiga shuti moja kali ambalo linamshinda golikipa wa Azam Razak na kuiandikia yanga goli la pili.
Azam 1, Yanga 2
Dakika 45 zinakatika na mpira ni mapumziko
Kipindi cha pili
45' Kipindi cha pili kinaanza
46' Faul inapigwa kwenda lango la Azam
48' Mashambulizi yanaendelea kwa timu zote mbili huku kila timu ikicheza kwa umakini mkubwa.
52' Rafael Daud anapiga kros moja lakini anakosekana wa kuimalizia
53' Azam wanapanga mashambulizi kwenda lango la yanga lakini Yanga wanakataa
55' Steven Kingwe anatoka na kuingia Mbaraka Yusuph
58'Azam wanalisakama lango la Yanga bila mafanikio.
60' Yanga wanafanya shambulizi la kushtukiza kupitia kwa Ibrahim Ajib lakini kipa anaiokoa.
63' Azam wanafanya mashambulizi mawili kwenye lango la Yanga lakini yanashindwa kuzaa matunda.
66' Azam wanamtoa Chilunda na kuingia Paul Peter, Yanga wanamtoa Emmanuel Martin na anaingia Gefrey Mwashiuya.
67' Azam wanazidi kulisakama lango la Yanga, Himid Mao anapiga shuti lakini linaenda nje.
68' Yanga wanamtoa Ibrahim Ajib na kumuingiza Juma Mahadhi.
69' Azam wanapanga shambulizi kwenye lango la Yanga lakini Ata Aggei anaharibu mipango kwa kupiga nje.
73' Azam wanafanya mashambulizi zaid kwenye lango la Yanga lakini hayajazaa matunda.
75' Papii shishimbi anapewa kadi ya njano anaoneshwa kadi ya njano kwa kutaka kupigana na mchezaji wa Azam.
77' Agrey Moris anaoneshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu mchezaji wa Yanga Obrei Chirwa.
79' Faul inapigwa na Calvin Yondan kuelekea lango la Azam
80' Juma makapo anapiga shuti kuingiza katika lango la Azam ;alomo
81' Salum Abubakar anaonyeshwa kadi ya pili ya njano na kuonyeshwa tena kadi nyekundu baada ya kumsukumu Hasan Kessy wa Yanga. Anatoka nje ya uwanja. Azam sasa wanacheza pungufu yaani 10.
84' Faul inapigwa kuelekea lango la Yanga
88' Mchezaji wa Yanga anagaragara chini baada ya kuumia.
90' Yanga wanafanya shambulizi kwenye lango la Azam kupitia kwa Juma mahadhi, Geofrey Mwashiuya anaipata lakini anashindwa kupachika wavuni.
90+2' Yanga wanapiaga faul lakini haijazaa matunda.
90+3' Na mpira umekwisha.
Azam 1, Yanga 2