Yes.. bao la Kwanza alipoteza umakini. Hesabu zake wakati akiufata mpira zilimwambia yuko nje ya eneo lake la 18.. Utaona alijaribu kufanya block badala ya kudaka. Ni uzembe wa kukosa umakini tu.
Upande wa pili lile ni aina ya bao linalokuonyesha tofauti ya Obrey Chirwa na mastraika wengi nchini. Juhudi, kujitolea na kunusa kila harufu ya hatari. Chirwa ni mtu hatari hata bila ya kuwa na mpira mguuni.
Sidhani kama ile tunayoiita "Pasi ya akili" iliyopigwa na Ajib, ingeteneneza bao kama sehemu ya Chirwa angekuwa amesimama straika flani hivi kutoka katika mitaa yetu ya Jiji la Dar es salaam.
Chirwa amejitengenezea bao lake! Thats all.
Bao la pili. Thats Wow! It was fantastic.. Brilliant.. Huwezi kumlaumu Abarola pale.. hata David De Gea angeomba maji ya kunywa baada ya ule mkwaju.
Rudi uitazame tena clip ya lile bao, Gadiel aliitazama, akajiandaa, akapiga...Ooh my God, Hakuna kipa anayeweza kufanya lolote shuti likinyooka kwenye angle ile. Individual brilliance.
Kuhusu Sure Boy, Hili lipo ndani yao Azam FC. Kama tutakiita kitendo cha Sure Boy ni "Ujinga" basi tusisahau kuwaita Azam "Wajinga" pia.
Mwalimu Stewart Hall aliwahi kuniambia, "Ambiere, niko tayari kumpanga Sure Boy kwenye mechi zote tutakazocheza na Simba, hata ziwe 10 nitampanga tu, lakini siwezi kujaribu kumtumia hata kwa dakika 1 kwenye mchezo dhidi ya Yanga"
"Kwanini," Nikauliza kwa shauku.
"Wachezaji wenu wamegoma kuwa Proffessional. Haya matatizo mnayajua na hakuna Mwalimu atakayekuja kuyarekebisha kwa usiku mmoja" Alinijibu Stewart na kuondoka zake.
All in All, Pointi 3 zimekwenda Yanga. Credit zake George Lwandamina... Aliuharibu mchezo kwa mbinu. Jinsi tulivyoona Yanga inacheza hovyo, ndivyo ilivyokuwa ngumu kwa Azam kutafuta nafasi. Wakaishia kupiga piga pasi nyingi kwenye nusu yao.
Bado Simba, Azam, Yanga, Singida United, wanaweza kuamua wanachotaka kukipata mwishoni mwa msimu. Ligi tamu hii. Ambiere Kamwe naweka nukta hapa.