Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Baada ya kusimama kwa muda ligi kuu soka Tanzania bara inarejea tena hiyo kesho tarehe 11 Februari, ambapo mchezo wa awali utakaopigwa saa 8: 00 mchana, utaikutanisha Kagera sugar dhidi ya Gwambina. Na baadaye Coastal union atamenyana na Azam Fc majira ya saa 10:00 jioni.
Ijumaa ya tarehe 12 kabumbu litaendelea kurindima ambapo Tanzania Prisons atakuwa mwenyeji wa KMC mchezo utachezwa saa 8:00, huku Ruvu shooting akimualika Ihefu mchezo utakuochezwa saa 10:00 za jioni.
Na wikiendi itaanza kwa michezo miwili, ambapo Mwadui Fc atashuka dimbani kukipiga na Biashara United majira ya saa nane mchana huku Mbeya city akipimana nguvu na watoto wa Jangwani Young Africans mchezo utaochezwa saa 10:00 jioni.