Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa Klabu ya Azam FC kukutana na Tanzania Prisons katika dimbani Nelson Mandela huko Mbeya
Mara ya mwisho Azam kukutana na Tanzania Prisons ilikuwa Septemba 26, 2020, katika mchezo ambao Azam ilikuwa ugenini na kufanikiwa kujiwekea kibindoni alama 3 muhimu baada ya kuitandika Prisons goli 1-0.
Mchezo mwingine utakao pigwa hii leo ni kati ya Dodoma Jiji ambayo itakuwa nyumbani kuialika Polisi Tanzania.
Tangu ligi kurejea tarehe 14 Februari, Dodoma Jiji imecheza michezo 2 na kufanikiwa kushinda michezo yote kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT Tanzania na Coastal Union.