Karibuni kwa Live updates kutoka dimba la CCM Kambarage Mjini Shinyanga
Moderator utanisaidia kuhariri/EDIT kichwa cha habari iwe Stand united vs Simba kwa maana Stand United yupo uwanja wa Nyumbani CCM KAMBARAGE
Mpira umeanza hapa...
Dakika ya 1...Simba wameanza kwa kasi Stand United nao wanaonekana kutulia kudhibiti mashambulizi
Dakika ya 7 Stand United wanafanya shambulizi hatari lakini Pascal Wawa anamsaidia Aishi Manula kudhibiti hatari hii
Dakika 5 ; Paul Bukaba anamchezea faulo mchezaji wa Stand United hapa inakuwa ni Faulu
Asante Kwasi Anapewa kadi ya Njano Dakika ya 12 baada ya kuachwa kichenga na Datus Peter
Dakika ya 13 bado ni 0-0
Stand United wanafanya shambulio Zuri hapa kupitia Jacob Massawe ila inashindikana pale mpira unatoka nje
Dakika ya 15 Simba wanafanya Shambulio hatari hapa linalosababisha Kona, mabeki wa Stand United pamoja na Golkipa wao wanatumia akili ya ziada kuokoa hatari hiyo
Timu zote hapa zinashambuliana kwa zamu na kwa umakini mkubwa sana...Wote inaonekana wamekamia mechi hii
Dakika ya 19 Adam Salamba anapiga shuti Golini mwa Stand United lakini Golikipa anaokoa hapa kwa umahiri
Dakika ya 24 Mackenzie Ramadhan wa Stand United anafanyiwa faulu hapa... (bado bao ni 0-0)
Dakika 32 Beki wa Stand United Ahmed Tajdin anaokoa shambulizi la john Bocco hapa...anakuwa mwepesi na mpira unatolewa hapa
Wakati huo John Bocco yupo chini anagaagaa maumivu...
madaktari wanamganga pale anafanikiwa kuinuka na kuendelea
Dakika 34 Stand United wanapata Kona kuelekea Simba, Majaliwa Shaban anamimina Krosi pale inakuwa ni kona nyingine...Kona hiyo inapigwa lakini inatoka nje...inakuwa goalkick
Dakika ni ya 36' Stand United wamesimama kidete kudhibiti mashambulizi ya Simba ambao wanakuja kwa kasi sana...
Dakika ya 38 Simba wanaonana Wawa, Dilunga na John Bocco ila Beki Ahmed Tadjin anavuruga mipango ile...... Stand 0- Simba 0
Dakika 40 Rashid Juma anafanya ujanja hapa ndani ya Box la Stand United kwa kujirusha akitegemea atapata faulu/penalti lakini refa anakataa pale...
Stand United wanatakata hapa, wanacheza pasi fupi fupi za kuonana
Dakika 43: Asante Kwasi anapiga mpira golini...John Bocco anapiga tik tak lakini mpira unatoka nje...Stand United walizubaa kidogo hapa kwenye marking
Dakika 44.John Bocco anashambulia pale kwa Juhudi Binafsi, anapiga shuti linambabatiza mchezaji wa Stand inakuwa kona kuelekea Stand United
Asante kwasi anapiga kona ndefu inaokolewa na Mabeki inatoka nje...Kona ya kurusha...
Dakika 4 za Nyongeza kuelekea Halftime..
Simba wanashambulia tena ila kipa Mohamed Makaka anauwahi pale
Dakika 45'+2 Meddie Kagere anaingia kuchukua nafasi ya Adam Salamba aliyetoka baada ya Kuumia
Majaliwa Shabani wa Stand United anashambulia pale lakini ananyang'anywa na beki za simba
Mpira muda wowote utaenda Mapumziko, Simba wanapata Faulo baada ya Gyan Nikolas kuwekwa chini.. Asante Kwasi anapiga Faulo eneo hatari pale lakini mpira unakuwa mwingi, Simba wanauwahi ...Dilunga anauwahi anaingiza ndani pale lakini inashindkana Meddie Kagere anacheza faulo.
Mpira ni mapumziko hapa CCM KAMBARAGE STADIUM
STAND 0- SIMBA 0
Karibuni tuendelee na kipindi cha pili hapa Kambarage Stadium
Mechi imeshaanza hapa....bado milango ni migumu kwa timu zote mbili
Dakika 47 kuelekea 48 Stand United wancheza vizuri lakin wanapoteana..Aish Manula anautokea na kupiga mbele... Unamkuta Dilunga anapiga krosi inakuwa ni goal Kick
Dakika ya 50 Simba wanapata Penalti kuelekea Stand United baada ya mchezaji wa stand united kuunawa kwenye eneo la Box
Gooooooal.... John Bocco anafunga Penalt dakika ya 52
Stand United 0 - Simba 1 (Bocco 52')
Simba inaonekana wamechachamaa wanashambulia tena hapa lakini inashindikana Stand United wamejidhatiti...Haruna Niyonzima na Said Dilunga wanaonana pale inakuwa ni Kona
Dakika 55 Kwasi anapiga kona ndefu kuuuubwa mpira unakuwa mwingi unakuwa ni wa kurusha kuelekea Simba
Dakika 56..Stand United bado hawajakata tamaa wanashambulia lango la Simba lakini Datus Peter anafanya faulo
Wakti huohuo Dakika ya 58 Jonas Mkude anaingia kuchukua nafas ya Rashid Juma... ( Stand United 0 - Simba 1)
Dakika ya 60. Tajudin anasimama vyema kwenye nafas yake anatoa pasi kwa mwenzake lakini inatoka nje, inarushwa kuelekea kwao Stand.
Mohamed Makaka anaokoa mpira ule langoni anaupiga ngumi unatoka nje kule...anawahimiza mabeki zake wajipange vizuri pale
Dakika 65 mabeki wawili hapa wa Stand united wanaucheza mpira ule unatoka.. ina kuwa ni kona inapigwa na Asante Kwasi... Gyan anaupata anampasia Bocco
Gooooooooaaaal Simba wanapata goli la pili hapa dakika ya 69 (John Bocco)
Dakika 71..William Kimanzi anaingia kuchukua nafasi ya Datus peter kwa upande wa Stand United
Dakika 73...pia Mwinyi Alex anaingia kuchukua nafas ya Morice Mahela kwa upande wa stand united
Stand United wanashambulia lango la simba hapa ila inakuwa ni Goal Kick
Stand United 0 Simba 2
Dakika 76.. Mwinyi Elias na Hafidhi Musa anapiga faulo kuelekea Simba pale.. hatari paleee lakini Aishi Manusa anaipangua..bado hatari...mchezaji wa Stand anapiga shuti lakini Aishi Manula anaudaka
Simba wanashambulia lango la Stand Niyonzima Kagere wanaonana wanampasia Bocco inakuwa ni goaal kick ikiwa ni dakika ya 79
Bado kama dakika 8 kuisha mpira...meddie kagere anaunawa mpira inakuwa ni faulo
Wakti huo Dilunga ametoka akaingia Mzamiru Yasini kwa upande wa Simba Sc
Dakika 85 Gyan Nikolas anaingiza Kross lakini Makenz Ramadhani anauwahi na kuondoa hatari ile langoni mwa Stand United..
Stand United wanajisahau, Shaban Majaliwa anaoneshwa kadi ya njano kwa kumchezea ndivyo sivyo Niyonzima....
Dakika ya 86-87 Stand United pia wanaanza kwa kasi pale Majaliwa shaban anazuiliwa na Nikolas Gyan..inakuwa ni wa kurushwa kuelekea Simba
Dakika ya 89 Haruna Niyonzima na Pascal Wawa wanaonana... Paskal Tadjin anaokoa..Kagere anaupata lakini Mwamuzi anakataa anamwambia kagere umefanya faulu
Dakika ya 90 sasa bado mpira unaendelea
Dakika 3 za Nyongeza.... (Stand United 0 Simba 2)
Muzamiru anaupaka mpira mafuta pale na anutoa nje inakuwa ni wa kurushwa kwa Simba...
Pascal Wawa anaukoa kwa shuti reefu linalozuiliwa na Tadjin beki wa Stand United...
Dakika 90+ 2 wakati huo Kagere anaukokota kwa Nguvu kuelekea goli la stand United, shambulizi lake halijazaa matunda..
Dakika 90+3' Mpira umekwisha kutoka Dimba la Kambarage CCM hapa mjini Shinyanga...
Stand United 0 Simba 2
Ahsanteni kwa kuwa pamoja nami katika matangazo haya mubashara...
Joseverest