LIGI KUU YA CHINA KUONYESHWA "LIVE" NA SKY SPORTS

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038


Sky Sports wameingia mkataba na ligi kuu ya China Chinese Super League kuonyesha ligi hiyo moja kwa moja kutoka China.

Mechi hizo zitaanza kuonyeshwa live kwa misimu mitatu mfululizo kuanzia jumamosi ya tarehe 30 julai mwaka huu hadi mwaka 2018.

Mechi ya jumamosi itakuwa ni kati ya Shanghai Greenland Shenhua na Jiangsu Suning.

Jumapili Guangzhou R&F watapambana na timu ambayo inafundishwa na meneja wa zamani wa England Sven Goran Eriksson ya Shanghai SIPG.

Msimu wa Chinese Super League unaanza mwezi March na kuendelea hadi mwezi November kila mwaka ikishirikisha timu 16.

Baadhi ya wachezaji aarufu mbao wametkea ligi mbalimbali duniani hasa ligi kuu ya Uingereza wanashiriki ligi hiyo.

Wachezaji hao ni kama Ramirezi kutoka Chelsea ambae anachezea timu ya Jiangtsu Sunning, Obafemi martins ambae aliwahi kuchezea Newcastle na sasa anachezea Shanghai Greenland Shenhua, Gervinho kutoka Arsenal na Roma ambae anachezea timu ya Hebei China Fortune FC na Graziano Pelle ambae juzijuzi amejiunga na timu ya Shadong Lundeng kutoka Southampton ya Uingereza.


Alex Teixeira na Ramires walihamia Uchina kwa ada kubwa za uhamisho.

Pelle pia anaungana na mshmabuliaji mwingine wa kutoka timu ya Newcastle ya Uingereza katika timu hiyo inayofundishwa na meneja wa zamani wa timu ya Fulham pia ya Uingereza Felix Magath.

Wachezaji wengine maarufu ni pamoja na Jackson Martinez ambae anachezea timu ya Guangzhou Evergrande, Alex Teixeira anaechezea Jiangtsu Sunning pamoja na Jo ambae aliwahi kuchezea Man City ya Uingereza, Ezequiel Lavezzi ambae sasa ni majeruhi, Stephanie M'bia ambae aliwahi kuchezea timu ya QPR ya Uingereza, na Demba Ba juzijuzi ameumia mguu wakati akichezea timu yake ya Shanghai Shenhua.

Wachezaji wengine ni wa kutoka Brazil ambao ni pamoja na Ricardo Goulart, Alan, Paulinho ambae aliwahi kuchezea Tottenham Hotspurs ya Uingereza, Hulk na Nikija Jelavic ambae anacheza kwenye ligi ya daraja la kwanza ya Beijing Rehne.

Ligi hiyo imekuwa kivutio kikubwa kwa wachezaji wa ligi kuu hasa za bara la Ulaya na mchezaji aliefungua mlango alikuwa ni Asamoah Gyan ambae aliposajiliwa na timu ya Shanghai SIPG kutoka timu ya Al Ain ya Qatar alikuja kuwa ni mchezaji wa sita duniani kwa kulipwa mshahara mnono.

Lakini Gyan hajaweza kuwa mahiriu katika ufungaji wa magoli jambo lililowafanya timu hiyo kumsajili Hulk kutoka Zenit St Petersburg.

Timu za China zimetumia zaidi ya Yuan bilioni 2 sawa na Euro milioni 299 zikiwa ni ada ya uhamisho wa wachezaji mbalimbali.

karibu katika uzi huu mahsusi kabisa kuhusu ligi ya Uchina.
 
Basi dstv nayo tutaona si ndg hawo sky sport na dstv nahisi mmiliki ni mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…