Baada ya kumalizika rasmi kwa msimu wa 2024/2025 mnamo Mei 25, 2025,
Ligi Kuu ya Uingereza (English Premier League) itaendelea leo kuashiria rasmi kuanza kwa msimu wa 2025/2026. Mchezo wa ufunguzi utafanyika majira ya
saa 4:00 usiku katika dimba la
Anfield, kati ya
bingwa mtetezi Liverpool na
Bournemouth.
Ligi ya Uingereza inajulikana kama moja ya ligi zenye mvuto mkubwa duniani, kutokana na wachezaji wake wenye kiwango cha juu na ushindani mkali. Takwimu zinaonyesha kwamba Liverpool imeibuka na ushindi katika
mechi 5 za mwisho walipokutana na Bournemouth, jambo linaloongeza hamasa kubwa kwa mashabiki.
Msimu huu pia umeongeza
timu mpya waliopanda daraja, ikiwemo
Burnley, Leeds United, na Sunderland, baada ya timu za
Leicester City, Ipswich Town, na Southampton kushuka daraja.
- Jumamosi:
- Aston Villa vs Newcastle
- Brighton vs Fulham
- Sunderland vs West Ham
- Tottenham vs Burnley
- Wolves vs Manchester City
- Jumapili:
- Chelsea vs Crystal Palace
- Nottingham Forest vs Brentford
- Manchester United vs Arsenal
Mashabiki wa Ligi Kuu ya Uingereza wanaweza kufuatilia michezo hii kwa shauku, kwani kila mchezo unahesabiwa na kila timu ina ndoto ya kupata ushindi katika msimu mpya.