Ligi kuu ya Tanzania inaendelea kukua siku adi siku

Calyx24

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2018
Posts
213
Reaction score
292
Wakuu kwakweli nimevutiwa kwa kiasi kikubwa na hamasa ya watanzania katika ligi kuu ya tanzania yani kwa kipindi hiki watu wamekuwa wakiangalia hata mechi za kawaida katika ligi ambazo hazina ushawishi kwa kiasi kikubwa kama inavyo julikana

Naweza kusema kuwa ligi ya tanzania ndio ligi inayoongoza kufatliwa na watu wengi yaani katika kuangalia mechi kwenye runinga ukiachilia mbali suala zima la kubeti tofauti na hapo awali ambapo ni mara nyingi ligi ya uingereza ndio ilikuwa ikiteka hisia kwa kiasi kikubwa sana kwa mashabiki wengi

Juzi nilipita kwenye ukumbi fulani ikanibidi niulize watu kuwa hapa mbona watu wamejaa sana walinambia kuwa watu wanaangalia mechi ya Simba na coastal union hakika nilishangaa sana kwa umati ule

Nawapongeza watanzania kwa kuendelea kuthamini vitu vyao vya ndani kwa kiasi kikubwa

NAWASILISHA
 
Basi tabia zenu wakenya mtaanza kusema hi ligi ya kwenu
 
nawapongez watanzania kwa kuendelea kuthamini vitu vyao vya ndani kwa kiasi kikubwa

NAWASILISHA
Kwa sisi wahenga tunakumbuka sana , "ligi ya daraja la kwanza" ilivyokuwa ikipendwa enzi zile za FAT.
 
League inakuwa na inalipa. ila viwango bado vidogo. Ukiwaondoa Kagere, Chama, Konde Boy,Morrison, Mkoko, Tuisila, Nahimana ligi inakuwa kama Ndondo
 
Ahsante sana, Tanzania kuna mashabiki wa kutosha yaani EAC nzima,ila tunaangushwa na viwango vya wachezaji wawapo ground.
 
Ni kweli inakua ila tatizo ni viwanja vibovu na mashabiki wa utopolo wanaopiga wanawake viwanjani. Hawajui kama wanawake huongeza mvuto viwabjani!!!!
 
Referees waongeze weredi wao kazini ligi itabamba sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…