Mkuu ligi inaendelea vizuri tu,ila tatizo inatawaliwa sana na vimbwanga ambavyo hata kujadili ni udhia mtupu:- Mara maiti imeibwa mortuary ili kulogea mechi,...ooo mara waganga 30 wamekwenda kuloga mechi Mwanza ..... sijui Ulimboka kaenda kumlipa deni Kado wakati kuna mechi inamkabili mbele na wadau kuhusisha na hongo,.... mara nyimbo za Taifa zimegoma kwenye cd.....blabla .... ooo Kaijage kasimamishwa kazi kumbe mkataba ulikwisha siku nyingi........ mara tenda ya tiketi za mechi bado kutangazwa huku ligi inaendelea na watu tunanunua tikets,....utakuta wenye uwezo wa kulipa viingilio ndo wanaoingia viwanjani bure kwa kisingizio eti ni wadau. Hapo utakuwa na hamu kweli ya kufuatilia ligi! Tunafuatilia kiugumu ugumu tukiamini kuwa haya yote yatakwisha.