Ligi Kuu ya Vodacom kuendelea kesho

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali, ikiwa inaingia katika raundi ya tisa huku kila timu ikisaka ushindi wa pointi tatu muhimu.

Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Simba SC watawakaribisha Coastal Union kutoka jijini Tanga, mchezo utakaonza majira ya saa 10:30 jioni, huku Ndanda FC wakiwa wenyeji wa Stand United uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Wachimba Almasi wa Mwadui FC watawakaribisha Yanga SC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Toto African watakua wenyeji wa maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Wakata miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar watakua wenyeji wa Kagera Sugar katika uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro, huku watoza ushuru wa jiji la Mbeya katika uwanja wa Sokoine Mbeya City watakua wenyeji wa Majimaji kutoka mkoani Ruvuma.

Ligi hiyo itaendelea siku ya Alhamis kwa michezo miwili kuchezwa, Tanzania Prisons watakua wenyeji wa African Sports katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, JKT Ruvu watakua wenyeji wa Azam FC katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
 
Kila la Kheri..

1. Simba S.C "Taifa Kubwa"
2. "Wana wa kukaya" Mwadui FC
 
Kati ya Simba na Coastal Union, kuna mtu anakula 2 bila
 
Kwel siasa inapendwa huu Uzi umedoda ile mbaya
 
mwadui 0 yanga 1 dk 12 goli kafunga donald ngoma
 
Matokeo ya mwadui na Yanga vipi mpaka sasa kwa aliye na taarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…