Ligi Kuu ya Wanawake: Simba Queens yaitandika Yanga Princess mabao 7-0

Ligi Kuu ya Wanawake: Simba Queens yaitandika Yanga Princess mabao 7-0

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi kuu ya wanawake 'Women's Premier League' iliyoendelea leo kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kwa kuwakutanisha watani wa Jadi upande wa wanawake, imeshuhudia Simba Queens ikiitandika bila huruma Yanga Princess mabao saba kwa bila.

Mchezo huo ulikuwa kusisimua kwa dakika zote 90 licha ya Simba Queens kutawala mchezo iliwachukua dakika 45 za kipindi cha kwanza kwenda mapumziko Simba Queens wakiwa mbele kwa mabao matatu

Mabao ya Simba Queens yaliwekwa kimiani na Mwanahamisi Omari aliyefunga mabao matatu Hat-Trick, pamoja na Amina Ally, Amina Ramadhan huku Frora Kayanda akijifunga (Og) upande wa Yanga Princess ambayo imepanda daraja msimu huu.




IMG_20190113_182629_170.jpeg
IMG_20190113_180837.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana kwa Simba Queens... Simba sasa inabidi waanze kuwaunga mkono kwa asilimia 100 hawa kina dada. Wako vizuri kiukweli!
 
Mtu kapigwa 7 unasema mchezo ulikuwa wa vuta nikuvute?
 
Tupe takwimu za kufungwa na kufungwa Kati ya Simba na Yanga,bila kusahau magoli mengi kafungwa nani na ubingwa kachukua nani mara nyingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Awamu ya Kwanza -nyerere ndala walipigwa 5 mtungi.

Awamu ya pili -mwinyi chura walipigwa 6 yai.

Awamu ya tatu-mkapa mbute walipigwa 5 bila

Awamu ya nne-kikwete makwasukwasu mkapigwa 5 nsajigwa anatembea na magoti, Okwi anamburuzaaa kama lotee.

Awamu ya tano-Eeeeee Mungu epushiaa mbali hiki kipigoooo kinachokujaaa Kwa hawa omba ombaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom