Ligi ya Europa: Manchester United kuvaana na AC Milan

Ligi ya Europa: Manchester United kuvaana na AC Milan

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105
IMG_20210226_174058_379.jpg
Manchester United itacheza na washindi mara saba wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, AC Milan katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Europa.

AC Milan, ambayo inashika nafasi ya pili katika Serie A, bado haijawahi kushinda mashindano ya Europa, wakati ushindi pekee wa United ulikuwa mnamo 2017.

Arsenal, iliyofika fainali mwaka 2019, itakutana na timu ya Uigiriki ya Olympiakos, ambayo iliitoa katika hatua ya 32 mwaka jana.

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic atarejea Old Trafford katika mchezo wa pili, wakati pande hizo mbili zitapokutana kwa mara ya 12 - mechi zote zilipokutana awali zilikuwa kwenye Ligi ya Mabingwa.

Ranger, iliyopata ushindi wa jumla ya goli 9-5 dhidi ya Royal Antwerp Alhamisi na kufikia hatua ya 16 bora kwa msimu wa pili mfululizo, itachuana na Slavia Praha kwa mara ya kwanza.

Wapinzani wa Tottenham, Dinamo Zagreb, itakayokuwa mwenyeji wa mchezo wa kwanza, wamepoteza mechi zao tisa kati ya 10 za mwisho dhidi ya timu za Uingereza kwenye mashindano ya Europa.
 
Back
Top Bottom