LIGI YA ITALY INARUDISHA UBORA WAKE

TAKE NOTE

Member
Joined
May 28, 2019
Posts
13
Reaction score
10
Baada ya miaka ya hivi karibuni ligi ya italy kupoteza ubora kama miaka ya nyuma ambapo timu za AC milan na juventus kuwa wababe wa ligi za ulaya pamoja na miamba ya Inter milan ligi hii ilipitia changamoto nyingi hadi kupoteza ushindani kwenye michuano ya ulaya na ubabe huo ukihamia katika nchi za spain na uingereza.
Vigigo wa ligi hiyo JUVE,AC milan, inter, roma wameanza kujidhatiti katika kufanya mabadiliko ya timu zao huku juve baada ya kumchukua Ronaldo ili awaletee UEFA na kuishia katikati ya safari wameamua kuboresha kikosi chake kwa kumchukua kocha wa chelsea Sarri ambae amekuwa kocha katika ligi hiyo kwa muda mrefu, ndugu zao Ac milan wameboresha bench lao kwa kubadili kocha wao hii inaonyesha sasa juhudi wanazo fanya ligi hii inarudisha ushindani wao wa muda mrefu.
 
Huyo Sari katoka hapo hapo Italy akiwa na Napoli kabla ya kwenda Chelsea je aliifikisha wapi Napoli? Ac milan bado wamekuwa waendelezaji wa kucheza kamari tu kwa kuchukua makocha wasio na uzoefu wakati wapo katika hatua ya kuijenga timu kurudisha kwenye ubora wao. Mauro Tassotti, Clerance Seedorf, Filippo Inzaghi, Mihajlovic, Brocchi, montella, na Gattuso wote wameshindwa kuirudisha Ac Milan kwenye ubora kutokana hawakuwa makocha wenye uzoefu. Kuja kwa Sari kunaweza kufanya Juventus ishuke na kuwa level moja na wakina Napoli na Inter milan au kunaweza kuendeleza gap iliyokuwepo kati ya juve na timu zingine za Italy. ila sioni kama hizi timu za Italy zikirejea kwenye kutoa changamoto kwenye soka la ulaya
 
Ubora bado sana kurudi mpaka timu za Milano zirudi.inter baada ya morati kuiuza kwa muindonesia anaitwa thohir hakuna kitu kilichofanya na yeye akaiuza kwa mchina.Ac milano berlusconi naye kawauzia wachina sijui wakina Sun bado hawapo vzr kwa sababu juventus familia ya agnelli hela wanazo na ndiyo maana wakajenga uwanja wao pia.hata kama wanaamua wachukue mchezaji kwa italia hamna anayemuweza.Napoli mwaka wa ngapi anashika nafasi ya pili? Roma imeuzwa kwa wamarekani mpaka leo nao hakuna kitu.l.na roma hata iwe mbele kwenye msimamo hata point 20 usiiamini ni kama Arsenal tu.timu ambazo juve atapata wasiwasi zikirejea kama zamani ni za Milano tu yaani AC milan na Inter milan, nazo zitachukua muda kweli kwakuwa waliozinunua wamenunua kwa maslahi yao binafsi siyo kwa ushindani na juventus.sasa hivi wachezaji wazuri anayeweza kununua ni juve peke yake.Wengine wanalalamika wanaema juve anabebwa na marefa ni kweli ila kama hawaonyeshi uwezo je.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…