Ligi ya Mabingwa Afrika: Simba SC 4-1 Mbabane Swallows

Ligi ya Mabingwa Afrika: Simba SC 4-1 Mbabane Swallows

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Posts
11,660
Reaction score
11,654
Kwa heshima kubwa kabisa Leo simba inaanza safari ya kimataifa na inaanza na timu kutoka uswetu

Nipo Taifa tayari kwa kuwaletea mpambano huu live

Tayari watu wameshajaa nje ya uwanja hamasa Ni kubwa Jezi zinauzika sana za simba

Kuna foleni kwa magari yanayotoka gerezani ila km kama unapitia mwembe yanga utafika bila usumbufu

Mechi itaanza saa kumi kamili jioni 16:00 kwa saaa za Afrikaans masharik I

14:15 Gari yenye wachezaji wa simba tayari yaingia uwanjani moja kwa moja kwenye dressing room

15:15 timu zote zimeingia uwanjani kufanya warm up

15:55 timu zinaingia uwanjani

Tajiri wa simba SC MO dewj anapewa heshima na mashabiki wa simba SC

dkk 10 boko.......... Simba anaandika goli la kwanza kupitia boko

dkk 14 swalos wanasawazisha

LA pili boko Tena kwa mkwaju wa penalty

Wakuu vitendea kazi vimeisha moto endelezeeni uzi

====

Ligi ya Mabingwa Afrika, Mpira umemalizika kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam, Simba wanaibuka na ushindi wa mabao 4-1. Mchezo wa marudiano utapigwa Desemba 5, mwaka huu nchini eSwatin.

FT: Simba SC 4-1 Mbabane Swallows.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa jumla ya mabao 4 – 1 dhidi ya Mbabane Swallows katika michuano ya klabu bingwa Afrika.

Katika mchezo huo John Bocco amefanikiwa kufunga jumla ya mabao mawili katika kipindi cha kwanza dakika ya nane na 32,kisha nyota wao Meddie Kagere akifanikiwa kufunga la tatu dakika ya 84 na Clatous Chama akihitimisha karamu ya magoli kwa kufunga dakika ya 90+2 huku lakufutia machozi la Mbabane likitiwa kimyani na Nzambe dakika ya 24.

Mchezo huo uliyokuwa wa kipekee kwa Simba umeshuhudia muwekezaji wao Mohammed Dewji akiwa miongoni mwa watu waliyokwenda kuwashuhudia uwanjani na kuwapa nguvu ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo toka apatwe na tatizo la kutekwa kisha kupatikana mwezi Oktoba mwaka huu.

Kutokana na matokeo hayo Mbabane Swallows watalazimika kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3 – 0 kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Simba ili kujihakikishia wanasonga mbele na kumtoa Mnyama.
IMG_20181128_182357.png
 
Kwa simba kila goti litapigwa
Aisee... Sasa nafuta sala zangu... Mpigwe goli 2... Na iwe FT SIMBA 0 - 2 MBBNE ...

Ewe mungu baba, mueza juu kila kitu, usiyeshindwa jambo lolote mbele yako, baba muumba mbingu na ardhi, na kila vilivyomo kwenye ulimwengu huu...
Nina ombi moja kwako leo baba... Baba naomba ujaalie timu ya simba ifungwe goli mbili tu wala sio yingi baba...
Baba hawa simba wanajikuta wao ni Barcelona ya Tanzania... Kumbe hawana lolote la maana... Timu imejaa wazee waongo wanaodanganya umri wao.. baba jaalia kabisa na wafungwe mechi ya marudiano...
Baba naamini umesikia ombi langu baba... Hakika wewe ni msikivu mwenye kujibu shida za wanyonge...

Aaamiiin
 
Wewe mla konyagi Sala yako inaelekea kibra

Back
Top Bottom