Ligi ya Mabingwa Ulaya: Chelsea uso kwa uso na Atletico Madrid huku Lazio wakiwakaribisha Bayern Munchen

Ligi ya Mabingwa Ulaya: Chelsea uso kwa uso na Atletico Madrid huku Lazio wakiwakaribisha Bayern Munchen

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105
20210223_111349.jpg

Michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya itapigwa hii leo ambapo, Atlètico Madrid ya Hispania atakipiga dhidi ya Chelsea ya England.

Michezo ambayo Atlètico Madrid amekutana na Chelsea katika mashindano ya Ulaya ilikuwa na matokeo sawa kwa timu zote, kila timu imeshinda mara 2 na kutoka sare mara 3.

Katika mchezo wa leo Chelsea atamkosa mchezaji wake aliyesajiliwa akitokea PSG Thiago Silva kufuatia kuwa majeruhi.

Huu ni mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa kwa Thomas Tuchel akiwa kama kocha wa Chelsea.

Diego Simeone hajawahi kupoteza nyumbani katika hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa tangu kuwa kocha wa Atlètico. Na Atlètico imewahi kufika hatua hiyo mara saba ndani ya misimu nane.

Hata hivyo, mchezo wa leo kutokana na ugonjwa Corona na Wageni kutakiwa kukaa Karantini wakiingia Uhispania, mchezo huo utapigwa katika dimba la Arena Națională, Bucharest, Romania huku Atletico ikiwa mwenyeji


Mchezo mwingine wa ligi hiyo utakaopigwa leo ni kati ya Lazio dhidi ya Bayern Munich.

Hii ni mechi ya kwanza ya ushindani kati ya Lazio na Bayern .Lazio imepoteza mechi moja tu kati ya sita za ligi hiyo dhidi ya timu za Ujerumani na hajawahi kupoteza nyumbani.

Na Bayern Munich haijafungwa katika mechi zao tano za mwisho za ligi ugenini dhidi ya timu za Italia.
 
Back
Top Bottom