Ligi ya Ukraine imerejeshwa. Ina maana maisha Ukraine sasa ni kama kawa?

Ligi ya Ukraine imerejeshwa. Ina maana maisha Ukraine sasa ni kama kawa?

ward41

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2022
Posts
749
Reaction score
2,533
Ligi ya Ukraine imerudi rasmi leo kwa mara ya kwanza tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mwezi Februari mwaka huu.

Kutokana na sababu za kiusalama, mashabiki hawakuruhusiwa kuhudhuria mechi ya kwanza iliyochezwa kati ya timu za Shakhtar na Metalist katika uwanja wa Kyiv Olympic.

Hifadhi za dharura zenye kuzuia mabomu zimewekwa tayari karibu na uwanja ikiwa zitahitajika.

Nahodha wa timu ya Shakhtar ameeleza kuwa "tunazo kanuni zetu ikiwa kengele italia wote tutaenda kwenye mahandaki"

"Tuko tayari, tuna nguvu, na nafikiri tutaionyesha dunia kuwa bado tupo, na kama wanavyofanya askari wetu nasi tunapambana kwa ajili ya Ukraine."
 
Kwan si urusi wanatupa mabomu kila Siku au? Hawaoni hiyo risk?
 
Unaweza kuua miili ya watu kwa mabomu lakini usiweze kuua spirit/mioyo yao. Hili ni tusi kubwa la nguoni kwa dikteta Putin 🤔
 
Sasa watarusha bomu kuwatandika warusi kutokea uwanjani mechi ikiendelea na warusi wakijibu tu wanabatizwa jina ni wauaji wa wachezaji na adui wa wanamichezo.

Warusi Wangeondoka tu nchini kwa watu watoe tangazo kuwa Ukraine ijijiunga NATo halafu USA na NATO ikaweka silaha mipakani mwa Urusi tunarusha nuclear kuelekea huko huko.
 
Jamaa kweli wahuni sana. Hurusha makombora kutoka hospitali, supermarket, shuleni, etc.
 
Back
Top Bottom