Likizo ndefu ya form 4 inakaribia, nimsaidie vipi huyu mhitimu mtarajiwa asipoteze muda wake kiholela mpaka vyuo vitapofunguliwa mwakani ?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Ninaishi na kijana hapa kwangu anakaribia kuhitimu form 4

Tulishapanga akimaliza form 4 aende chuo, (sijaona faida ya form 6 nje ya kozi za afya)

Ninakumbuka enzi zangu nilipoteza sana muda baada ya kumaliza form 4 - ntaamka saa moja ntafanya kazi za nyumbani hadi saa tatu baada ya hapo hakuna cha kufanya zaidi ya Kusikiliza muziki, kwenda kijiweni , kucheza game, jioni ntaenda kucheza mpira, kuangalia movie, n.k. Mpaka naingia kidato cha tano hakuna chochote nilichogain

Ni kitu gani kizuri kinaweza kuwa msaada kwake.
 
Chochote kati ya hizi au vyote vikiwezekanika mkuu.Muda wa kumaliza f4 kusubiria tokeo ni mwingi mno atakuja kujutia badae wakati angejifunza skills za kumpush mbele kidogo.
1.Driving course basic apate hata leseni class D.
2.Computer basics(Microsoft word,excel,powerpoint)
3.Graphics designing.
4.Computer ICT,IT short courses
5.Language study kama ni mfuasi wa lugha mojawapo kubwa duniani kama Fluent english,basic germany,basic chinese,basic french or spanish.

Nikikumbuka zingine ntakurudia mkuu.
 
 
Mkata uzi kumbe zimozimo eehh,ukiwa humu kuna wakati unajizima data.Sasa na kupa ushauri wa bure,Mfundishe angalao lugha moja ya kimataifa kwa gharama sawa na bure!Down load app inayoitwa Dualingo chagua lugha yeyote inayoweza msaidia na kumnufaisha kwenye maisha yake,laa ajifunze matumizi sahihi ya AI yenye manufaa.Ila katika usimamizi na uangalizi kwani inahusisha matumizi ya vifaa vya kidigitali.
 
Thread # 5 kamaliza kila kitu.. asome lugha hasa Kifaransa ...muhimu sana hili kwa dunia ya sasa
 
Mpeleke VETA akapate kujifunza stadi za za ufundi.
 
Mtihani hata bado hawajafanya, wee ushajua hadi matokeo, Lol
 
Mpeleke veta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…