ndugu wanaJF naomba mnisaidie kuhusu sheria za kazi zinasemaje kwa hii tetesi ninayo isikia,.Mimi ni mtumishi wa MAMLAKA YA RELI YA TANZANIA NA ZAMBIA(TAZARA) ambapo kwa kipindi kirefu sana imekuwa ikijiendesha kwa hasara inayo sababishwa na urasimu pamoja na rushwa inayo lipelekea kushindwa kilipa mishahara ya watumishi kwa mda mrefu sana ikafika kipindi ambapo Waziri Nundu alifikia kipindi cha kuwasimamisha wakurugenzi saba kwa tuhuma mbalimbali lkn waziri alietangulia Dr Mwakyembe aliwarudisha kwa kigezo cha kukiukwa kwa taratibu za kisheria,sasa kuna tetesi kuwa Mamlaka imeshindwa kujiendesha na kukwama kwenye masuala muhimu ya kiutawara ambapo inazamilia kutoa likizo kwa baazi ya wafanyakazi wake bile malipo,.naomba mnisaidie kwa wanasheria kuhusu suala la Mwajiri kumsimamisha mafanyakazi wake mwenye mkataba wa kudumu na shirika kusimamishwa bila ya malipo,.