Lile Jambo linazidi kupingwa, ajenda kuu Misa ya Pasaka

Lile Jambo linazidi kupingwa, ajenda kuu Misa ya Pasaka

Fortilo

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
5,807
Reaction score
17,416
Ndio, nazungumzia lile Jambo,

Limekuwa agenda kuu Misa ya Pasaka..
Wazazi wapaswa kuwajibika kulea maadili ya watoto wao.

Hili jambo wengi tunalivamia lakini ukwel ni kwamba kwa Tanzania mkakati ulianza zamani sana..

Angalia hapa..
1. Kabla ya mwaka 2005 kulikuwa na fursa Sawa kwa wote.... aka break the read tape

2.Miaka ya 2005 kuja had 2015 ikaja Wanawake na maendeleo...aka women empowerment

3. 2016 kuendelea iakaja Haki Sawa kwa wote, aka role play.., wanaume wakaanza kushona sare, kwenda clinics, kupewa likizo za uzaz nk...

4. 2020 kuendelea ni public promotion and advocacy....

Kuna mkuu mmoja huko North kafungia Dagaa mmoja kujihusisha na jambo hilo, asilojua fedha ni nyingi sana na wanufaika ni wengi mno akiwemo yeye.

Baba wa Mababa wa jambo hilo wapo Dar es salaam, conscience inakataa lakini mwili ni dhaifu.... muda wi mrefu vigezo vitawekwa kila mahal Ili tupate funding.

Kuua tunu za familia na kudidimiza nguvu za wanaume makusudi.

Leo Kanisa limestuka... lile jambo limeanza kuwa agenda kwenye nyumba za ibada, ni agenda kuu Misa ya Pasaka.

Hata kumkataa shetani na mambo yake yote imekuwa ngumu.... tunamkataa Lakin mambo yake tunafanya.... huo ndio mtego.

Mtesi wetu ana nguvu sana, tusali mambo ni magumu mno.
 
Ni Jambo zuri hii movements kwenye nyumba za Ibadan..
Changamoto ni Taasisi za dini zenye makao makuu Ulaya ambako huko wameanza kuhalalisha
Mkuu upo saahih kabisa... hatar ninayoiona...

Dini karibu zote zina makao makuu kwenye hizo nchi za baridi ambako wao wamekubali kulieneza kwa nguvu.

Kanisa la Afrika likikataa fedha tukazingatia maadili na tunu zetu, Mila na Desturi tunaweza zuia angalao kizazi hiki kikapona.
 
waache unafiki wajikite kwenye ufufuko wa Yesu tu, kuongelea lile jambo itakuwa ni unafiki wa kisiasa tu wakati ngoma ilishajikita mizizi siku nyingi, it is too late wanapopoa matatawi wakati shina lipo na lina mizizi migumu kuing'oa ni shughuli pevu.

Kuna wengine wa ule upande wao wanakurupuka na maandamano yao bila kutafiti ni wapi mbegu ya mmea huo imetoka ikaja kupandwa kwetu ikaota na kustawishwa kwa kupewa huduma zote mmea zinazotakiwa mmea kupata ili ustawi na ukue na hatimaye utoe matunda tayari kwa kuvunwa.

Zilianzishwa harakati za kipuuzi sana na kupewa kampeni nyingi mpaka zingine zilitungiwa sheria zenye adhabu kali. Jamii iliona sawa tu haikujua ndani yake kuna agenda za kuvunja maadili ya familia, malezi na ndoa.

Sasa jamii inalia kilio cha mbwa koko kuhusu jambo hilo ambalo awali haikujua nini kitatokea mbeleni. Kazi ipo, unafiki uachwe
 
kilio eti tufuate mila zetu, upuuzi mtupu, tutafuata mila zetu zipi hizo wakati hazipo tulishaachana nazo kitambo? Tena mila zingine zilikuwa nzuri katika kutunza maadili ya ndoa na familia zikaundiwa kampeni na kupata ufadhili toka nje, miradi ikaanzishwa na kusukumwa na kampeni kali kutomeza mila hizo kisha sheria kali zikatungwa kukomesha mila hizo ambazo kimsingi zilikuwepo ili kulinda maadili kwa jamii.

Upuuzi mtupu, unabomoa misingi ya maadili ya watu wa taifa lako, yakitoweka unaanza kulialia maadili yafuatwe, yako wapi hayo maadili ya taifa letu.

Kosa kubwa lilifanyika la kuvunjavunja misingi ya maadili haikupaswa kuingiliwa na kuguswa kilimbukeni kwa tamaa ya kupata fedha za wahisani wa miradi ya kuvunja maadili yetu.

Watu walifanya mambo hayo kulinda mila na tamaduni za maadili yao wakajitokeza wanaharakati wapuuzi wakapiga kampeni eti mila hizo ni kandamizi kwa utu. Wakaingia mpaka vijijini kuharibu maadili ambayo jamii iliweka ili kulinda maadili ya familia na ndoa. Ndoana huwa na chambo
 
Hebu acheni kuzungumzia jambo hili sana, mi naona linavyozungumziwa zaidi ndio tunazidi kulipa nguvu
 

Attachments

  • Screenshot_20230409-104807_Twitter.jpg
    Screenshot_20230409-104807_Twitter.jpg
    131.7 KB · Views: 5
Back
Top Bottom