Lile ni goal au siyo goal?

Lile ni goal au siyo goal?

RAMAJ

Member
Joined
Sep 24, 2018
Posts
88
Reaction score
89
Ni kama kasumba ya mipira inayoelekea golini kugonga kwenye mstari wa goal inaendelea kuwa mwiba mchungu kwa timu ya Yanga. Tena katika mechi muhimu ambazo wanahitaji matokeo ya ushindi. Ukianza na mechi baina ya Mamelod na Yanga, mpira uliyopigwa na Aziz Ki na kugusa mstari wa goal ulizua taharuki katika kila kona ya Afrika kwa waliofwatilia mechi ile. Hawa wakisema lilikuwa ni goal, na wale wakisema halikuwa goal, lakini uhalisia ulibakia kwenye filimbi ya muamuzi aliyeamua kuwa "Halikuwa goal"

Zimwi hilo hilo limeendelea kuwatafuna tena siku ya leo, ambapo team ya Yanga ilikuwa ikipepetana na JKT Tanzania katika uwanja wa General Isamhuyo, mpira ambao ulipigwa krosi na kumkuta Guede na kuusukumizia golini bahati mbaya, uligonga post na ulivyoshuka chini ukagusa tena post ya pembeni tena katika mstari wa goal. Muamuzi akaashiria kuwa halikuwa goal.

Bahati mbaya sana picha za marejeo hazikutupa angle zote kutuonesha kuwa je, ulivuka au haukuvuka? Sote tumebaki kwenye kigugumizi, je mpira uliingia golini au haukuingia?

Matokeo yamesalia kuwa Yanga 0:0 JKT Tanzania.
 
Je wajua La liga hawana goal line technology?
=======

Kuhusu Yanga sijafuatilia mechi yao, mamanyeto alikuwemo?
 
Sio goli mbona ilikuwa wazi kabisa, Mpira umegonga nguzo kwa chini ukarudi uwanjani.
 
Nilicho na uhakika nacho ni kwamba kwa kila goli analo dhurumiwa Yanga, simba atalilipia wakati fulani
 
Ni kama kasumba ya mipira inayoelekea golini kugonga kwenye mstari wa goal inaendelea kuwa mwiba mchungu kwa timu ya Yanga. Tena katika mechi muhimu ambazo wanahitaji matokeo ya ushindi. Ukianza na mechi baina ya Mamelod na Yanga, mpira uliyopigwa na Aziz Ki na kugusa mstari wa goal ulizua taharuki katika kila kona ya Afrika kwa waliofwatilia mechi ile. Hawa wakisema lilikuwa ni goal, na wale wakisema halikuwa goal, lakini uhalisia ulibakia kwenye filimbi ya muamuzi aliyeamua kuwa "Halikuwa goal"

Zimwi hilo hilo limeendelea kuwatafuna tena siku ya leo, ambapo team ya Yanga ilikuwa ikipepetana na JKT Tanzania katika uwanja wa General Isamhuyo, mpira ambao ulipigwa krosi na kumkuta Guede na kuusukumizia golini bahati mbaya, uligonga post na ulivyoshuka chini ukagusa tena post ya pembeni tena katika mstari wa goal. Muamuzi akaashiria kuwa halikuwa goal.

Bahati mbaya sana picha za marejeo hazikutupa angle zote kutuonesha kuwa je, ulivuka au haukuvuka? Sote tumebaki kwenye kigugumizi, je mpira uliingia golini au haukuingia?

Matokeo yamesalia kuwa Yanga 0:0 JKT Tanzania.
Ni goli lakini sio goli
 
Back
Top Bottom