KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Nikiwa ktk lindi la usingizi mwanana ambao haukuwa na tone la dosari huku nikiwa kungwi nilietopea ktk aina ya ndoto zakijasusi!,ambazo uhusika wangu Mimi huwa ni sterling nisiepigwa na ikitokea nimepigwa basi nasitisha!..
Ktk hali ya sintofahamu leo kichwa changu kimebadili mkondo wa ndoto!,leo nimetumbukia ktk lile joho nililoliona watu kadhaa humu ndani wakilisimulia kama zimwi la ndege kuanguka!.
"Ni ghafla from no where nilikuwa ktk mazingira ninayoyafahamu ikiwa ni mchana tena ktk mkoa ambao ni chaguo langu namba moja!, nipo na baskeli yangu mara ghafla naangalia hewani naiona ndege kubwa ya abiria ikienda mlama!,mlio wake uliashiria hali ya hatari ambapo ndani ya muda huo ilionyesha dhahiri si abiria Wala pilot wote walijawa na taharuki!.
Hofu ilinitanda sana nikajikuta nasimama na baskeli yangu nakuanza kufatilia tukio lile lakuogofya!,ndege iliendelea kutapatapa huku ikijaribu kutokomea machoni pangu lkn kabla haijapotea kwa asilimia zote nikaona jambo jengine lakushangaza!.
Ndege ileile ilibinuka yani matairi yakaelekea juu hata pia ikabadili uelekeo ikaanza kurudi ilipotokea! Ikiwa inatapatapa ikawa inashuka huku ikienda mbali nami! Hapo hofu ilikuwa imenitanda huku nikiimagine wanachopitia watu waliokuwa ndani yake!.. punde ikapotea machoni pangu nakuanguka chini! Nilisikia kelele tu nakuona moshi!...!
Nikijua yameisha kumbe hayajaisha ndege nyengine ndogo nayo nikaiona ikiwa imebinuka kama Ile kubwa!,ikienda mlama kufuata ilipoangukia Ile kubwa nayo ikaanguka pia! Japo sikujua kama iliangukia palepale ilipoanguka Ile kubwa!.
Nikiwa ktk huzuni na tafrani iliyojawa kivumbi na jasho,punde mbele yangu nikaona kundi la wamama wakiwa na watoto wao wakitembea huku wakipiga stori hawana hiyana na Wala hisana! Ni kama walikuwa hawajui hatari yoyote Ile iliyotokea!.. walikuwa wakitembea nakuja mbele yangu na ndipo hapohapo tukio jengine likatokea!....
Nikaanza kusikia nakuona milipuko toka uelekeo wa airport ya mkoa huo!.. Hali ilikuwa tafrani nikaona bora niikimbize nafsi yangu isije kupokwa na zimwi hili la ndege na milipuko!.
Na ndipo hapohapo nikadamka kutoka usingizini huku nikishangazwa na aina hii mpya ya uotaji wangu na ndipo nikakumbuka visa viwili vilivyoletwa humu ndani ambavyo naona vinafanana kabisa na hii ndoto yangu!!! Ndo Sasa najiuliza hili zimwi limenipata namimi au ni kiherehere changu tu!!!😅