Lilisemwa, Waziri Akapinga--Lakini Sasa Latimia

SolarPower

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
223
Reaction score
27
Katika kikao cha Bunge kinachoendelea Dodoma kuna Mbunge mmoja alizungumzia tetesi kuwa Serikali imeamua kuanzia mwaka huu (2011) mtihani wa Hisabati wa Darasa la Saba utakuwa wa Multiple choice lakini Waziri wa Elimu na Naibu wake walipinga. Lakini ukweli ni kuwa hivyo ndiyo ilivyoamuliwa na ndivyo itakavyokuwa kwani watoto waliofanya mtihani wa Moko mwezi huu wa saba katika somo la Hisabati majibu yake yalikuwa ni Multiple Choice. Na matokeo ya uamuzi huu mbovu yameanza kujitokeza kwani katika shule moja kuna wanafunzi ni dhaifu sana katika Hisabati lakini wamepata maksi ambazo zimewashangaza hata walimu wao.

Chama cha hovyo huunda serikali ya hovyo na matokeo yake viongozi wake wa hovyo hufanya maamuzi ya hovyo.

Tangu lini hisabati ikageuka kuwa jiografia ama historia? mtihani wa hisabati kuwa "multiple choice" ni uwendawazimu.

Hawajui maana ya hisabati hao vilaza wa wizara ya elimu nini??

ccm mapunguani kweli kweli... elimu yetu itaendelea kudidimia kila siku

Tatizo siyo huo uamuzi, tatizo ni utunzi wa hayo maswali yawezekana ni hovyo!! Ndo tatizo la kuiga kila kitu bila kukaa chini na kuhusisha watu walipoteza muda wao mwingi kwenye maisha yao wakisomea haya mambo ni laana tu! Huwezi ukasomea uhandisi wa umeme then ufundishe udaktari wa meno au watoto. Na ndiyo tuko hivyo wabongo.

Wakatae wasikatae nchi hii inahitaji emergency state, wataalamu, wanasiasa wakae chini waongee kuundwe Taasisi moja nyeti yenye kuainisha mwelekeo wa taifa ambao hata itokee nini lazima ufuatwe. Vinginevyo, ni upuuzi tu.

Kuna haja ya lazima kwa Chama cha Walimu Tanzania kupinga na ikiwezekana kuitisha mgomo nchi nzima. Serikali ya CCM inaipeleka nchi pabaya sana. Kama taifa hatupaswi kukaa kimya katika suala zito kama hili.

Nakubaliana na wewe. Ila kwa hali yoyote ile ni upuuzi uliovuka mipaka kutoa mtihani wa Hisabati wa Multiple Choice.

Inasemekana shule zote za msingi zimeshapewa agizo hili. Kipindi hiki waalimu wako bize kuwaandaa watoto kubahatisha. Taifa linakwisha. Naomba tuweke kumbukumbu ili tahehe hiyo ya 7 Septemba, ikikutwa ni hivyo, waziri awajibishwe kwa kulidanganya taifa.

labda wamegundua kuwa wenye uwezo watapeta na vilaza wachache wataweza kubahatisha.wakati mwingine ili mtu afanikiwe anahitaji bahati pia.huwezi jua labda hao vilaza wanaweza wakawa wakali wa baadaye.

Hapo ni kuwapa watoto mbinu za kuangalizia tu kwa jirani na kuwapa uwezo wa ziada kutambua kama jibu ni A au B au C kwisha mchezo. Mmezidi kuwalaumu kuwa watoto wanafeli wameamua kutumia njia ya mkato kufaulisha. Mbona haya JK hajui hesabu na aliwahi kukiri kuwa zinamgonga kikwelikweli sasa hao watendaji wake watafurahia hesabu. Kamwe nchi hii haitakuja compete kielimu kwa njia hizi za mkato

Ndio maana mwanafunzi anafaulu std 7 wakati hajui hata kuandika jina lake. Hawa Curriculum developers wamekaa kisiasa zaidi.

Hahahha nchi hii haishi maigizo .

Baadae watakuja na takwimu kuwa idadi ya wanafunzi kufaulu imeongezeka. Kwa elimu ya sasa usishanage kuna watoto wanafika darasa la tatu hawajui kusoma au kuandika.

Hahahha nchi hii haishi maigizo .

Baadae watakuja na takwimu kuwa idadi ya wanafunzi kufaulu imeongezeka. Kwa elimu ya sasa usishanage kuna watoto wanafika darasa la tatu hawajui kusoma au kuandika.

Mkuu si la tatu sema form 4 mtoto hajui kuandika sentensi wala kusoma!walisema mtihani darasa la 4 na form 2 upo lakini mtoto asirudie darasa akifeli marks 21.kwa ujumla mfumo wa elimu tanzania hovyo kabisa

Kweli kijana hapo juu ni balaa. Umenichekesha kweli kwamba hata mkuu wa inchi kakili kua hisabati kiboko. Mm nashindwa kuelewa hivi hata huko kwenye wizara kunawataalamu wengi inakuwaje wanakubali huu upuuzi wa ajabu. Nchi hii wanaimaliza kabisa kwan watoto wao wanasoma huko kwenye academia wakati sisi ndotunakomaa na kayumba zetu. mm nazani hata chama cha walimu wasikubali kwan huu ni upuuzi wa hali ya juu.

Mimi nilisoma somo la statistics nje Ulaya. Kwenye somo hilo tulikuwa wanafunzi 1500. Masuali yote yalikuwa multiple choice na waliopasi walipasi na waliofeli walifeli.

Jee unaweza kupata jawabu sahihi bila ya kufanya calculations kwanza? Na kwa kufikiria tu unaweza kupata jawabu moja au mbili lakini siyo zote.

hao waliofaulu wanajua KUTABIRI

mmmmh..! Hata kukiwa na multiple choices, ni lazima uumize kichwa kukokotoa,na uibuke na jibu sahihi,unless otherwise, hakuna kitu hapo..! Hahaha,ila dah, hii inanikumbusha matriculation xam ya udsm mwaka07,basic maths ya multiple choices,af imagine mtu aliesoma hkl ataambulia nini kama sio kuotea..! We have got a long way to go...

na secondary kuanzia mwakani. Semina ilishafanyika Mbezi

Nimeuona huo mtiani, i was shocked kwa jinsi elimu inachezewa! Sasa multiple mpaka Maths, tutapata mainjinia kweli? GOD HAVE MERCY ON US

Ccm oyeee.
Kwa elimu ya kiduanzi namna hii lazima Wakenya watuache mbali

Jaman, Ee! Tusibakie kulalamika tu na kunyamaza kwa ajili ya ujinga na upuuzi wa ccm, tuwatoe madarakani, tumechoka upuuz wao.

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…