Wapendwa wa jukwaa hili pendwa la MMU,
Ningependa kuchukua fursa hii kuwajulisha kwamba, mwenzetu Lily Flower amefiwa na kaka yake wa kuzaliwa.
Tukiwa kama rafiki zake, ndugu zake, tuungane nae katika msiba huu, tukimuombea moyo wa uvumilivu wa kuweza kukabiliana na wakati huu mgumu uliopo mbele yake kwa sasa.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi
Amen.
Msiba uko wapi? Biblia inasema ombolezeni na wanao omboleza, tutakuwa sio marafiki wa kweli uwapo tutakuwa tunaombolezea kwenye intanet wakati mwenzetu hajafiwa ki intanetintanet. Wenye nafasi twendeni tukamtie moyo, tukamfariji, tukakae nae sakafuni. Naomba mnipe physical address mi niende, kama msiba uko hapa DSM.